SHULE SOFT YASHAURI SHULE ZOTE KUJIUNGA NA MFUMO WA 'SHULESOFT' ILI KUONGEZA PATO LA NCHI.

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

KAMPUNI ya Shule Soft imezishauri shule zote nchini ambazo hazijajiunga na mfumo wa ShuleSoft kujiunga ili kuweza kumpunguzia mhasibu mzigo wa kazi kwa kutumia Teknolojia.

Amesema kuwa kupitia mfumo wa ShuleSoft mzazi anaweza kulipa ada kupitia simu na pia mhasibu kupokea malipo moja Kwa moja kwa njia ya control namba na kutoa risiti ya TRA ambapo pia itasaidia kuongeza Pato la Nchi.

Hayo yameelezwa na Afisa wa fedha wa kampuni ya Shule Soft Upendo Onesmo katika mkutano wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika Jijini Dodoma.

Kupitia mfumo huu kwa kiasi kikubwa inasaidia kuongeza pato la Nchi na kupunguza faini ambazo zinapigwa na Mamlaka husika na kupata taarifa sahihi

Vilevile kulikuwa na changamoto moja ambayo karibia shule zote walikuwa wanapitia pale ambapo mzazi anamsomesha mtoto na ikatokea mzazi akapata changamoto ya kifo au ulemavu wa kudumu hii ni ngumu sana kwa shule kumfukuza mtoto kwaiyo kinachotokea pale shule inakuwa inamsomesha mtoto bure,

Sasa tulichokifanya tumeweza kujiunga na Insurance Company inaweza kumsaidia yule mzazi pale ambapo amefariki au anapata ulemavu wa kudumu na mtoto anaendelea kusomeshwa moja kwa moja na Insurance Company kupitia ShuleSoft na akasoma mpaka akamaliza,"alisema.

Amesema kuwa kupitia ShuleSoft mzazi anaweza kuona taarifa za matokeo ya mwanafunzi, taarifa za ada pamoja na matangazo yanayotolewa na shule anayosoma mtoto.

Tumeweza kumsaidia mzazi kuongeza uhusiano wa mzazi na shule, mzazi atapokea matokeo kupitia mfumo huo na anaweza akatoa maoni ambapo akitoa maoni yake yanafika moja kwa moja mpaka shule

Maoni hayo yatamfikia mwalimu wa somo husika, Mwalimu Mkuu wa shule pamoja na Mwalimu wa darasa na hii itapelekea Mwalimu na mzazi kusaidia kuona ni namna gani wanamsaidia mwanafunzi na afanye vziri katika masomo na kuongeza idadi ya watu ambao watalisaidia Taifa letu mbeleni,"alisema.

ShuleSoft ni mfumo ambao unapatikana mtandaoni (online) pale ambapo shule inataka kujiunga inatakiwa kuwa na Mtandao (internet) pamoja na kifaa ambacho kinaunganisha na mtandao huo (internent) mfano Kompyuta mpakato, simu ya mkononi au kishkwambi na aina nyingine ya vifaa vya kielektroniki ambavyo vinaweza kutumika.

Mfumo ukiwa uko sawa unaweza kutumika sawa na wazazi wanavyotumia Mitandao ya kijamii kama Facebook,Whatsapp na mitandao mingine ya kijamii.

 

Post a Comment

0 Comments