SERIKALI YASHAURIWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

SERIKALI imeshauriwa kutenga na kuelekeza fedha katika miradi ya mabadiliko tabianchi kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa katika sekta za nishati jadidifu, kilimo ikolojia, miundombinu na kilimo himilivu.

Hali hiyo itasaidia taifa kuwa na usalama wa chakula na kujenga uhimilivu endelevu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Rahma Kiriwe, mwanaharakati wa mabadiliko tabianchi na mazingira, amesema hayo jijini hapa, wakati akisoma ripoti ya uchambuzi wa fedha za miradi ya mabadiliko tabianchi ambazo zimekuwa zikiingia nchini uliofanywa na Jukwaa la vijana la Global Platform Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Action Aid Tanzania.

Kiriwe, amesema Tanzania kama yalivyo mataifa mengine Duniani imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazifanani kati ya nchi na nchi jamii na jamii nyingine lakini pia athari hizo hutofautiana katika ya watoto na watu wazima, vijana na wazee.

Ikumbukwe kuwa jitihada za kidunia za kuhimilina kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi zinahitaji Rasimali fedha na tayari kuna makubaliano ya Kimataifa kuhusu upatikanaji na matumizi ya fedha hizo

Aidha, amesema inapaswa kutenga na kuelekeza fedha katka sekta na idara zinazosimamia majanga na namna ya kukabiliana na majanga hayo kwa ustawi wa jamii na uhimilivu dhidi ya majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

Pia, serikali kuhakikisha mahitaji mahsusi ya vijana katika mkutadha wa mabadiliko ya tabianchi yanajumuishwa katika mipango na fedha zinazotengwa kwa ajili ya kukabiliana na athari kuanzia ngazi za vijiji/mitaa, wilaya hadi ngazi ya Taifa.

Akizungumzia uchambuzi huo amesema umejumuisha vijana kutoka mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Pwani, Tanga na Kigoma.

Kadhalika kulikuwa na wawakilishi wa serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usiamamizi wa Mazingira (NEMC) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa TAMISEMI kwa lengo la kuchambua kwa kina ripoti ya uchambuzi wa fedha za mabadiliko ya tabianchi hapa Tanzania

Amesema uchambuzi umebaini kuwa Tanzania inapokea fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya Kimataifa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kuhimili na kukabiliana na athari za mbadiliko ya Tabianchi.

Amesema kwa mujibu wa uchambuzi huo, asilimia 54 ya fedha zilizopokelewa zinatumika kutekeleza miradi ya kujenga uhimili dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kilimo, misitu, uvuvi, mazingira ya bahari, mazingira na uhifadhi wa baioanuai. 

Amesema matokeo haya yanawiana na vipaumbele vya serikali katika mipango na mikakati iliyopo.

Kadhalika, amesema uchambuzi umebaini kuwa serikali kupitia bajeti za kisekta inatenga fedha na kutekeleza miradi himilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Washiriki wamepata nafasi kujadili na kufanya tathmini ya matokeo ya ripoti kutoka kwa vijana kuhusu uchambuzi wa fedha za mabadiliko ya tabianchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Maji, Mazingira ya Bahari, Misitu na na Mazingira kwa ujumla ili kushawishi utekelezaji na ufanisi wa mtiririko na matumizi ya fedha za mabadiliko ya tabianchi katika sekta hizi nchini Tanzania

Vile vile, amesema lengo la uchambuzi huo ni kufahamu upatikanaji na matumizi ya fedha za mabadiliko ya tabianchi katika sekta hizo kwasasa ili kupendekeza maboresho, kuendeleza na kuleta suluhisho kwa vikwazo ikiwemo mfumo mzima wa ufuatiliaji wa matumizi kwa njia endelevu nchini.

Kimkakati, Umuhimu wa uchambuzi huu ni kuielimisha jamii ikiwemo vijana jinsi fedha za mabadiliko ya tabianchi zinavyopatikana na kutumika kwa ufanisi katika sekta hizo tano ikiwa ni moja ya juhudi zinazofanywa na wadau mbali mbali ikiwemo Green Climate Fund (GCF) ili kujenga uhimilivu na kukukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa Tanzania

Mratibu wa Program za vijana wa Shirika la ActionAid Tanzania Arif Fazel, amesema ipo haja kwa serikali kuendelea kutumia vizuri fedha za mabadiliko tabianchi zinazoningia nchini kwenye kilimo ikolojia ili kuwa na usalama na uhakika wa chakula.

Pia serikali itenge fedha kwa ajili ya kusaidia wakulima ambao wamekuwa wakiathiriwa na mabadiliko tabianchi pia kujengea uwezo vijana ili kuleta mabadiliko chanya

Arif


 

Post a Comment

0 Comments