SERIKALI imesema imepokea malalamiko yote
kutoka kwa Asasi za Kiraia na mashirika yasiokuwa ya Kiserikali (AZAKI)kuhusu
suala la kodi wanazotozwa ili hali hawafanyi Biashara yoyote.
Mamlaka ya Mapato itayafanyia kazi kujiridhisha na hoja zilizoletwa na wenzetu wa AZAKI
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Uchambuzi wa Sera na Utafiti kutoka Wizara ya fedha Bw.William Mhoja alipokuwa kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Kikodi kwenye Asasi za Kiraia(AZAKI) leo Oktoba 3,2023 Jijini Dodoma.
Mhoja amesema kutokana na hilo watafanya vikao vya mara kwa mara ili kusudi pasiwepo na malimbikizi ya changamoto ambazo wao wanaziona kama zimejitokeza na mpaka sasa wamezichukua.
Amesema kwa zile Asasi zilizowasilisha maombi ya kutokuwasilisha Return zao kwa wakati huku wakijua hawajafanya Biashara, wameomba msamaha kwenye maeneo hayo na suala hilo linahitaji maamuzi makubwa hivyo wameyachukua pia na wanaenda kuyafanyia kazi ili waone kama kuna haja ya kutoa Tax Amnesty.
Kamishna huyo amesema wao kama Serikali wamejipanga kuimarisha mfumo wa Mapato Ili kuhakikisha wateja wanapata huduma ipasavyo na kwa wakati zaidi.
Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Bw.Onesmo Olengurumwa amesema kwa mwaka huu 2023 Asasi za Kiraia takribani Elfu 1000 zimeingiza Shiling Trilioni 2 hivyo ni sekta kubwa ambayo imekuwa ikisaidia Serikali katika kuendesha miradi mbalimbali nchini.
Hii ni TASAF ya Wananchi kama ilivyokuwa kwenye upande wa Serikali, maana hii Wananchi kupitia Asasi zao wameona kuna changamoto ya kijamii wametengeneza taasisi zao, wanatafuta wahisani kwaajili ya kutatua hizo changamoto
Olengurumwa amesema wao kama sekta isiyojipatia faida wana umuhimu wa kukaa na Serikali kurekebisha Sheria zao ili waweze kwenda sawa katika kila jambo
0 Comments