SEKTA YA KILIMO NDIO IMEAJIRI ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA

 ðŸ“Œ JASMINE SHAMWEPU

NAIBU kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana ajira na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema sekta ya Kilimo ndio sekta pekee iliyoajiri watu wengi ambapo asimia 60 ya  Watanzania wamejikita kwenye Kilimo. 

Kutokana na uwepo wa kundi hilo kwenye sekta ya Kilimo serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeongeza nguvu katika sekta ya Kilimo kwa kuongeza Bajeti ya Kilimo hadi kufikia Billion 900

Katambi ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma wakati akifunga mdahalo kuhusu vijana na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo ulioandaliwa na bodi ya wadhamini na Menejimenti ya Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko (AMDT). 

Aidha katika hatua ingine amewata Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafikia wakulima wadogo ambao wamekuwa wakiongezea thamani bidhaa zao ili bidhaa wanazoziuza ziwe zenye ubora. 

Amesema katika maeneo mengi ambayo ametembelea, TBS imekuwa ikilalamikiwa kutowafikia vijana wajasilimali kwa wakati na kutoa mashariti magumu ambayo yanachukua muda mrefu  hivyo watoe elimu  ya namna ya kufikiwa ili bidhaa wanazozitengeneza zipatiwe vipimo kwa wakati.

Aidha, Katambi amesema Serikali imeanzisha mafunzo ya kilimo cha kisasa ambapo jumla ya Vijana 13,088 wamepatiwa mafunzo kati yao vijana 12,580 ni wa mafunzo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba, vijana 234 ni wa mafunzo ya kunenepesha mifugo, vijana 200 ni wa mafunzo ya ufugaji samaki na viumbe maji, na vijana 74 ni wa kilimo cha mazao kwa njia ya vizimba.

Nimepata Malalamiko kutoka kwa Vijana kuwa wanatengeneza bidhaa na kusambaza sehemu mabilimbani bila kuthibitishwa na watu wa Shirika la Viwango hivyo niwaagize nendeni mkawaone vijana hawa.

Katambi

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu  na Meneja Miradi, Ufuataliaji na matukio (AMDT) Athuman Zuberi amesema lengo la Mdahalo huo wa Vijana na Fursa kwenye sekta ya Kilimo ni kuwakumbusha ili waweze kuchangamkia Fursa zilizopo kwenye sekta ya Kilimo . 

Ukweli ni kuwa Vijana wengi hapa nchini wamejibweteka na hawazitambui fursa zilizopo kwenye Kilimo hivyo ni wakati wa Vijana kujikita kwenye Kilimo

Hata hivyo amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza nguvu nyingi kwenye Kilimo lengo Vijana kujikita kwenye Kilimo. 




 

Post a Comment

0 Comments