NBS YASEMA IDADI YA WATALII YAONGEZEKA NCHINI

 ðŸ“Œ.RHODA SIMBA

MKURUGENZI wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa amesema katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2023 imeonesha idadi ya watalii imeendelea kuongezeka hadi kufikia 1,131,286 ikilinganishwa na watalii 900,182 katika kipindi kama hicho mwaka 2022 hiyo ikiwa ni sawa na ongezeko la watalii 231,104.

Aidha kati ya watalii wote walioingia nchini kwa kipindi hicho kupitia Zanzibar ni 236,047 ambao ni sawa asilimia 31.1 ya watalii wote.

Masolwa ametoa takwimu hizo leo Oktoba 9 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia Milioni 1.5 ifikapo mwezi Disemba mwaka huu

Masolwa anasema idadi kubwa ya watalii kutoka nje ya Bara la Afrika waliotembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini wametoka nchi ya Marekani ambao idadi yao ni 84,541 ikifuatiwa na Ufaransa, Ujerumani Uingereza na Italia.

Nchi ya Kenya imeongoza kwa idadi kubwa waliotembelea Tanzania ambao idadi yao ilikuwa 128,753 ikifuatiwa na mataifa ya Burundi, Zambia, Rwanda na Uganda

 

Post a Comment

0 Comments