CHUO
Kikuu Mzumbe kimesaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za
Kitaaluma na Teknolojia na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA) kwa lengo
la kuendelea kuboresha huduma za Kitaaluma na Teknolojia zinazotolewa
Akizungumza
wakati wa zoezi la kusaini makubaliano hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
Mzumbe, Prof. William Mwegoha ameeleza kuwa sehemu ya Mpango Mkakati wa Chuo ni
kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuongeza wataalamu katika kutoa huduma za
kitaaluma ili kuongeza idadi ya wanafunzi na kukuza ufanisi wa programu
zinazotolewa na Chuo. Hivyo makubaliano hayo yatasaidia kubadilishana uzoefu na
ujuzi kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA).
Awali
akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi la kusaini mkata huo, Kaimu Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Chuo Kikuu
Mzumbe, Dkt. Eliza Mwakasangula, amesema makubaliano hayo ni matokeo ya Mkutano
wa tatu wa TEHAMA uliofanyika Jijini Arusha kuanzia Februari 8 -12, 2023
ukiratibiwa na eGA.
Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe umeona fursa na kupitia mradi wa Elimu ya Juu Kwa Mageuzi ya Kiuchumi upande wa Kujenga Ushirikiano wa Kazi na Sekta binafsi, Chuo Kikuu Mzumbe kimepata nafasi ya kuingia makubaliano hayo kwa maendeleo ya Taasisi na taifa
Dkt. Mwakasangula.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali
Mtandao, CPA Salum Mussa, amekishukuru na kukipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa
hatua ya kuboresha na kuimarisha mashirikiano na kuwa miongoni mwa Taasisi za
elimu ya Juu zinazoshirikiana na eGA moja kwa moja. Kwa niaba ya uongozi wa eGA
CPA Salum Mussa, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha
malengo yaliyokusudiwa katika mkataba huo yanafikiwa.
1 Comments
...Ni hatua zaidi teknolojia kurahisisha utendaji kazi
ReplyDelete