📌BARNABAS KISENGI
MAPEMA leo tarehe 11 Oktoba, 2023 viongozi wa kamati ya siasa ya Kata ya Kilimani pamoja na wajumbe wa Sekreatarieti ya kata ya Kilimani wamefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya msingi unaotekelezwa katika mtaa wa Chinyoyo kata ya Kilimani, Pamoja na kuona kasi ya ujenzi huo unavyokwenda
Viongozi wamesisitiza ujenzi huo uzidishwe kasi kulingana na mkataba unavoelekeza licha ya kuwa na changamoto ndogondogo ambazo hazizuii mradi huo kuendelea
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani Nathani Chibeye amesema ujenzi huo wa shule ya msingi hiyo utakuwa mkombozi kwa kata ya Kilimani kwakuwa kata hiyo tangu ipate Uhuru haijawahi kuwa na shule ya msingi jambo ambalo hupelekea watoto wa mitaa mnne ya Kilimani kusoma katika shule za kata nyingine na kusababisha kutembea umbali mrefu kutafuta elimu.
Sisi kama viongozi wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutupatia fedha za ujenzi wa shule hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata ya Kilimani
Chibeye.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Rotta Ndimbo ameitaka kamati ya ujenzi na mkandarasi kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo zinatumika kama zilivyokusudiwa.
Ziara hiyo ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani ni mwendelezo wa kugagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya Kilimani ili kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama unafanikiwa.
0 Comments