HAKUNA SABABU ZA KUWAKEKETA WASICHANA TUACHANE NA MILA ZENYE MADHARA-WAZIRI

 ðŸ“ŒWMJJWM, DSM

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Riziki Pembe amesema hakuna sababu ya kuendelea kukiuka haki za binadamu na ukatili kwa wanawake na wasichana kutokana na mila zenye madhara.

Mhe. Pembe ameyasema hayo wakati akihitimisha mkutano wa pili wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya kutkomeza ukeketaji uliofanyika jijini Dar Es Salaam Oktoba 9-11, 2023.

Amesema mikakati madhubuti iliyowekwa katika maazimio ya mkutano huo yataleta mabadiliko kwa kizazi kijacho katika kupambana na Ukeketaji.

Jambo hili si tu linakiuka haki ya msingi ya wanawake na wasichana bali pia ni ukatili mkubwa ambao sote tunakubaliana kwamba haukubaliki

Waziri Riziki

Ameongeza kwamba teknolojia itumike kuwakutanisha wadau wote na kubadilishana mawazo ya kutekeleza maazimio waliyojiwekea ili kutokomeza kabisa ukeketaji Afrika na Duniani kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq akizungumza katika mkutano huo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinalindwa kwa kukubali Programu za kutokomeza ukeketaji zinasimamiwa.

Hapa Tanzania juhudi mbalimbali zimefanyika tangu mwaka 1990 hatimaye Sheria ya kupinga ukeketaji ilitungwa mwaka 1998 na katika kuendeleza mapambano Serikali imeandaa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukeketaji pamoja sheria ya mtoto

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamesema makubaliano yaliyopatikana kwa pamoja watayafikisha katika Mamlaka za nchi zao ili hatua ziweze kuchukuliwa katika kupambana na kutokomeza vitendo vya Ukeketaji Afrika.

 



Post a Comment

0 Comments