SERIKALI
imewasilisha Bungeni azimio la kujiunga na Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa
Nishati Jadidifu (Statute of the International Renewable Energy Agency -
IRENA).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewasilisha azimio hilo leo October 31 bungeni jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ametaja manufaa mbalimbali yatakayopatikana baada ya kujiunga na mkataba.
Kuimarika kwa mchango wa Nishati Jadidifu katika uzalishaji wa Nishati ya Umeme nchini na kutaliwezesha Taifa kuwa na vyanzo mchanyanyiko vya umeme unaoendana na mahitaji ya ukuaji wa kiuchumi na kijamii
Aidha Biteko ametaja manufaa mengine kuwa ni kuimarika kwa uwekezaji, mitaji na upatikanaji wa ushauri wa kiufundi katika uendelezaji wa nishati jadidifu na kupungua kwa uharibifu wa mazingira unaotokana na uzalishaji na matumizi ya nishati isiyo rafiki wa mazingira na pia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kuimarisha kasi ya utekelezaji wa matumizi ya vyanzo vya nishati visivyoathiri mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi kuendana na mwelekeo wa dunia wa sasa
Amesema kwa kuzingatia manufaa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itayapata kutokana na Mkataba huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 12 na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, linaazimia kuridhia Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu Kuhusu ushirikiano wa kiuchumi.
0 Comments