CHAMA Cha wafugaji Tanzania (CCWT) kimesema ili kuendelea kutatua migogoro na changamoto ya wafugaji nchini kinakwenda kuzindua kadi za wafugaji na kuwasajili kutoka kwenye kadi za karatasi na kwenda kwenye kadi za kielektroniki ili kutengeneza kanzi data itakayowasaidia katika kazi zao.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 26 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CCWT Taifa Mrida Mshote Marocho wakati Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano wa uzinduzi wa kadi hizo Oktoba 28.
Kwasababu sasa tunahitaji kujua wafugaji wetu wanapatikana maeneo gani,na idadi yao ni wangapi maana kumekuwepo na changamoto nyingi ya migogoro kati ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi wakiwemo wahifadhi
Sisi kama chama tumekaa tukaangalia kwamba tukipata kanzi data hiyo itatusaidia kwa kiwango kikubwa sana na tunatamani siku ya uzinduzi wafugaji wengi waweze kujitokeza,"amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mipango na fedha Taifa(CCWT)Mathew Masele amesema kuwa baada ya uzinduzi huo wameagiza kila kanda watakuwa na vijana 2 kila Kata kwaajili ya kufanyiwa mafunzo na kukabidhiwa vishikwambi kwaajili yakwenda kuwaorodhesha wanachama katika maeneo yao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya malisho na migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi Tanzania Sir George Kifuko amesema kuwa wafugaji wanasahiliwa ili watambulike na itasaidia wao kujieleza Serikali idadi ya wafugaji waliopo pamoja na maeneo yao na changamoto zinazowakabili.
Mwanasheria wa CCWT Adv. Mathew Mtemi amesema kuwa lengo kubwa la chama icho ni pamoja na kutetea maslahi na haki za wanachama ambao ni wafugaji kupitia lengo hilo chama kina idara ya wakili ili kutetea haki za wanachama wote.
0 Comments