WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Boniface Simbachawene amewataka waajiri
kuhakikisha wanasimamia na kuimarisha uzingatiaji wa maadili ya viongozi
na watumishi wa Umma.
Ameyasema hayo leo Septemba, 21 jijini Dodoma alipokua akizungumza na wadau wa usimamizi wa maadili Katika Utumishi wa Umma na kusisitiza kuendelea kujenga ushirikiano wa usimamizi wa maadili Katika Utumishi wa Umma.
Wajibu wa kusimamia Maadili ya Watumishi wa Umma na Utawala Bora katika Utumishi wa Umma ni suala mtambuka ambalo liko chini ya Ofisi yangu kwa kiwango kikubwa, kwa kusaidiana na Taasisi Simamizi za Maadili na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma.
Hivyo, kwa kuzingatia dhamana mliyopewa katika kusimamia Maadili, mnapaswa kuendelea kushirikiana na kuwekeza katika mikakati ambayo itachangia kukuza Uwajibikaji na Usikivu wa watoa huduma kwa wananchi hususani katika maeneo yanayoigusa jamii moja kwa moja au kulalamikiwa mara kwa mara. Maeneo hayo ni pamoja na sekta ya Afya, Elimu, Ujenzi, Ardhi, Manunuzi na Ugavi
Simbachawene
Aidha Simbachawene amesema malengo mahsusi ya kikao kazi hicho ni kubadilishana uzoefu na taarifa zinazojumuisha mafanikio na changamoto za usimamizi wa maadili katika Utumishi wa Umma.
Ofisi yangu itaendelea kushirikiana na mamlaka ya usimamizi wa maadili ya kitaaluma na kutoa ushauri wa kitaaluma pale utakapohitajika kutoa ushauri katika mapitio na maboresho ya kanuni za maadili za kitaaluma
Simbachawene.
Katika hatua nyingne Simbachawene amesema Taasisi Simamizi za Maadili na Utawala Bora pamoja na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma ni miongoni mwa Taasisi ambazo hupokea malalamiko mbalimbali kuhusu ukiukwaji wa Maadili ya Utumishi na ya Kitaaluma, hivyo Mwongozo wa Ushughulikiaji wa Mrejesho wa Wananchi wa mwaka 2023 utasaidia kuimarisha utaratibu wa kushughulikia mrejesho kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi hizo.
0 Comments