WAZIRI wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Mhe. Selemani
Jafo ametoa pongezi kwa Rais ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa mjumbe wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi
duniani
Akizungumza na vyombo vya habari amesema ofisi ya
makamu wa rais wana dhamana ya kusimamia masuala yote ya mazingira na hivi
karibuni miaka mitatu mfululizo kulikuwa na mikutano iliyofanyika Glasgow
nchini Scotish, Sauhadsch nchni Misri na mkutano wa Africa Climate Summit
uliofanyika Kenya pamoja na majukwaa mbalimbali ya kidunia na Dkt Samia Suluhu
Hassan amekuwa kiongozi wa mfano sana katika suala zima la usimamizi wa
mabadiliko ya tabia nchi duniani.
Alisema utekelezaji wa Rais Samia Suluhu Hassan umeainishwa
kwa jinsi nchi yake ilivyojipambanua katika suala zima la kupambana na
mabadiliko ya tabia nchi kupitia miradi mbalimbali na Tanzania inapigiwa mfano
katika mradi wa ujenzi wa reli ya SGR itakayotumia umeme na itapunguza suala
zima la emmision ambayo Tanzania inatumia fedha zaidi ya shilingi trilioni 23
zimewekezwa katika mradi huu ambao kazi yake kubwa ni kupambana na mabadiliko
ya tabia nchi lakini mradi wa mabasi yaendayo kasi katika jiji la Dar-Es-Salaam
umejipambanua sana.
Mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar-Es-Salaam umejipambanua sana na duniani inaaminika kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi inayotiliwa mfano katika utekelezaji wa mabadiliko ya tabia nchi lakini hata hivyo uwekezaji mkubwa wa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 3 sawasawa na shilingi trilioni 6.5 ambazo zinawekezwa katika mradi wa Bwawa la Nyerere ambao utazalisha zaidi ya megawati 2115 na miradi hii yote kimataifa inaonekana ni miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi
Hivi karibuni mmeona kazi kubwa Mh. Rais amefanya ndani ya miaka miwili mfululizo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022-2023 uwekezaji mkubwa wa kuhamisha bajeti ya Wizara ya kilimo kutoka shilingi bilioni 294 mpaka bilioni 950 eneo hilo kubwa sana amewekeza katika suala kubwa la miradi tunaita smart agriculture kupeleka katika miradi ambayo itawezesha suala zima la adaptation kutengeneza miradi itakayoendana na uhimili wa mabadiliko ya tabia nchi
Jafo.
Aliongeza kwa kusema bajeti ya hivi karibuni ya mwaka wa fedha 2023-2024 zaidi ya shilingi bilioni 970 kutoka kwenye shilingi bilioni 294 mpaka hivi sasa ni kazi kubwa sana na eneo hili Mh.Rais amejielekeza haswa kwenye ujenzi wa Marambo ambayo shilingi bilioni 214 zitatumika kutengeneza Marambo 114 ambayo ni kazi inayomuonesha Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika suala zima la kujipambanua katika miradi ya mabadiliko ya tabia nchi..
Ofisi ya makamu wa rais tunapenda kumshukuru sana na
kumpongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuteuliwa kwake kuwa
mjumbe wa bodi ya mabadiliko ya tabia nchi duniani ambayo inaitwa GCA (Global
Center Adaptation) ni pongezi kubwa na tunapoelekea siku ya maadhimisho ya
Ozoni duniani Tanzania tuna jambo la kujivunia
0 Comments