WAZIRI wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana
amewapongeza viongozi wa dini nchini kwa juhudi zao za kuendelea kupambana na
vitendo vya ukatili na kuahidi kuwa, Serikali itaendelea
kushirikiana nao vyema katika kuhakikisha vinatokomezwa katika maeneo yote
nchini.
Dkt. Chana ameyasema hayo leo Septemba 22, 2023
Jijini Dodoma alipotembelea Ofisi za Tume ya kurekebisha sheria Tanzania na
kupokea taarifa mbili za namna Ofisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Amesema katika mashirikiano hayo wanapaswa kuzingatia
vyema sheria na taratibu walizojiwekea na wakishindwa kufanya hivyo watakuwa
wanafanya jambo ambalo sio sawa na wale waliopewa dhamana ya kusimamia eneo la
katiba na sheria watimize wajibu wao.
Tutaendelea kuwakumbusha watanzania, tutaendelea kutoa elimu tuzingatie taratibu fikiri sehemu ambazo mmejiwekea taratibu lakini mwingine anafanya kazi mwingine anaiba mali alizotafuta mwenzake yaani anaenda anachukua tu hiyo sio sawa, mwingine anapita tu mwingine anachukua panga anamtwanga tu hii haiwezekani tuna taratibu zetu
Dkt. Chana.
Aidha ameongeza kuwa hawatovumilia watu wanaovunja
sheria na kuvikumbusha vyombo vya ulinzi mahali popote ambapo watu hawataki
kufuata utaratibu ambao umewekwa wasisite kutoa taarifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha
sheria Tanzania Jaji Mstaafu January Msofe amesema kuwa utafiti kuhusu makosa
ya maadili ulibaini kuwa makosa hayo yamekuwa yakiongezeka nchini ambapo mwaka
2021 jumla ya makosa 7601 ya kubaka na kulawiti yaliripotiwa na mwaka 2022 makosa
8413 yaliripotiwa.
Hata hivyo kesi zinazofunguliwa mahakamani ni chache kuliko zile zinazotolewa taarifa katika vituo vya polisi matharani katika kipindi cha 2021/22 na 2022/23 ofisi ya taifa ya mashtaka ilifungua mahakamani kesi 2980 na 4294 mtawalia za makosa dhidi ya maadili yakiwemo ya ukatili, kubaka, kujaribu kabaka, kulawiti, na kujaribu kulawiti
Jaji
Mstaafu Msofe.
Jaji Mstaafu Msofe ameongeza kuwa taarifa zionesha
kuwa kuna kesi kubwa za makosa dhidi ya maadili ambazo hazijaripotiwa katika
vyombo husika.
Naye Katibu Mtendaji wa tume hiyo Griffini Mwakapeje amesema kuwa jumla ya ripoti zilizowasilishwa serikalini ni 56 na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo tume inaweza kufanya uchunguzi wa sheria yoyote ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuiendeleza.
Kwa kuelekezwa na wewe Waziri au mwanasheria mkuu wa serikali tume inaweza kutoa ushauri wa kisheria au msaada wa kisheria pale inapobidi na inapotekeleza majuku haya tume inaweza kufanya mashirikiano na taasisi nyingine za serikali na binafsi halafu na kutoa taarifa zake
Mwakapeje.
0 Comments