WANAOSAFIRISHA TAKA HATARISHI WATAKIWA KUZINGATIA MATAKWA YA SHERIA YA MAZINGIRA NA KANUNI ZAKE.

📌SUZANA ALEX & RUCIANA NYONI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Selemani  Jafo amelitaka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, kushirikiana na vyombo na Mamlaka zote za udhibiti zilizopo mipakani ili kuhakikisha shehena yoyote ya taka hatarishi ikiwemo chuma dongo inazingatia masharti na kanuni ya usafirishaji nje ya Nchi.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokua akizungumza na vyombo vya habari Septemba 22 na kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka mkazo mkubwa katika suala la uwekezaji wa viwanda vya ndani kwa lengo la kuzalisha ajira na kukuza uchumi.

Usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za chuma chakavu ikiwemo chuma dongo (cast Iron) nje ya nchi kiholela na usiofuata utaratibu unaweza kusababisha upungufu wa malighafi kwenye viwanda vinavyotumia malighafi za aina hiyo hapa nchini kwaajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo nondo na bomba za chuma

Jafo .

Aidha Mhe Jafo ametoa Rai kwa wananchi na wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya taka hatarishi hapa nchini kuzingatia matakwa ya Sheria ya mazingira na kanuni zake.

Kwa yeyote anayejishughulisha na shughuli za kukusanya,vkuhifadhi, kusafirisha ndani ya nchi, kuingiza nchini, kusafirisha nje ya nchi na kupitisha nchini taka hatarishi bila kibali, atakuwa ametenda kosa la kisheria na atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria

Jafo.

Kupitia usafirishaji wa  taka hatarishi nje ya Nchi zipo tozo, ada na Kodi zinazopaswa kulipwa, hivyo usafirishaji wa taka hizo bila kibali husababisha serikali kukosa mapato yanayopaswa kulipwa kupitia usafirishaji huo.

  


Post a Comment

0 Comments