DUNIA ikiwa inaadhimisha siku ya kichaa imethibitika kuwa kati ya wagonjwa 1000 watakaong'atwa na mbwa mwenye kichaa ni mgonjwa mmoja au wawili pekee ndio wanaoweza kupona.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa usimamizi wa huduma za ununuzi wa ugavi Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge na uratibu Mh. Arbogast Waryoba kwa niaba ya katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge na uratibu alipokua akizungumza na wananchi katika kilele cha siku ya kichaa cha mbwa Septemba 28,2023 Mpwapwa Jijini Dodoma na kusisitiza mbwa wafungiwe ndani wakati wa mchana kwani wanaweza kupata maambukizi endapo watakutana na wanyama walioambukizwa.
Amesema kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu jumla ya watu 20,005 walitolewa taarifa ya kung'atwa na wanyama na mikoa ambayo Takwimu zake zimechukuliwa na inaongoza kwa matukio ya kung'atwa na mbwa ni Dar es salaam 3321, Dodoma 3136, Morogoro 1159, na Arusha1155 Takwimu hizi zinajumuisha wananchi waliopata huduma katika vituo vya Afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Kinga Dkt.Rogath Kishimba amesema kichaa cha mbwa ni tatizo na ni rahisi zaidi kuzuia ikiwa kwa wanyama kuliko binadamu, kuzuia ugonjwa kwa maana ya chanjo ni gharama ndogo sana lakini kuzuia ugonjwa huo ukiingia kwa binadamu ni gharama kubwa sana.
Katika wagonjwa 1000 watakaothibitika na kichaa cha mbwa wanaoweza kupona ni mmoja au wawili kikubwa tuzingatie utoaji wa chanjo
Kishimba
Naye Mwakilishi wa Wizara ya elimu nchini na Afisa elimu Gerald George amesema haitokua mwisho wa elimu kuhusiana na kichaa cha mbwa itaendelea kutolewa
Ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni magonjwa yanayoathiri maeneo mengi duniani na ugonjwa huu husababishwa na kirusi cha kichaa cha mbwa (Rabies Virus)
Maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa hufanyika kila tarehe 28 Septemba ya kila mwaka duniani.
0 Comments