MSEMAJI
wa Timu ya wanawake JKT QUEENS Masau Bwire amesema wachezaji wote walioshiriki katika mashindano ya CECAFA
na mashindano ya ndani ni wachezaji
halali wa JKT QUEENS ambao
wamesajiliwa kwa usajili unaotambulika na TFF mpaka CAF.
Bwire
ameyasema hayo alipozungumza na CPC BLOG Jijini Dodoma na kubainisha kuwa mchezaji
yeyote anayechezea timu fulani huyo ana usajili uliokamilika tayari.
Wachezaji wote ambao tumewatumia katika mashindano yote tuliyocheza ni wachezaji halali wenye usajili unaokubalika uwe wa mkopo wa muda mrefu bado ni usajiri unaotambulika ndio maana wakacheza kama kusingekua na usajiri wachezaji hawa wasingepata fursa ya kucheza
Bwire.
Pia ameongeza
kwa kusema wanataka
waonyeshe kupitia timu
yao ya wanawake watanzania
wanaweza kufanya vizuri
kwani timu hiyo haina wachezaji wa
nchi za nje na badala yake wote ni wazawa
na hivyo wameweza kushinda
ligi kuu ya
wanawake Tanzania.
Sasa tunataka tuonyeshe na huku upande wa wanaume wapo watanzania wenye uwezo wana vipaji na kila sababu ya kucheza na kupata mafanikio makubwa na tukiwathamini wachezaji na kuwapa maslahi yanayoridhisha kama ambavyo tumekuWa tukifanya kwa wachezaji wa nje hivyo wanaweza kufanya jambo kubwa
0 Comments