WAZIRI wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini Mh Antony Mavunde amesema kuwa atahakikisha anatatua changamoto wanazo pitia wafanyabiashara wa eneo hilo ili kujiendeleza Katika biashara zao.
Waziri Mavunde ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mavunde katika kata ya Chang'ombe jijini Dodoma.
Nilitoa ahadi ya kuliimarisha soko letu hasa kwa wale wanaofanyia biashara eneo la mwishoni bidhaa zao zilikuwa zinaharibika na jua lengo langu nataka kuona soko hili linakuwa bora na soko lenye viwango vya hali ya juu
Mh Mavunde.
Aidha, Waziri Mavunde ameeleza kuwa wafanyabiashara wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya mitaji katika kuendeleza biashara zao hivyo ana mpango wa kuwaunganisha na Taasisi zinazokopesha ili waweze kuongeza mitaji yao na kujikwamua kiuchumi.
Kuna Taasisi ya (Sokoni Microfinance) nimeishawishi kuja kufanya biashara Dodoma imeanza Majengo sasa hivi Nkuhungu kutoa elimu juu ya utoaji wa mikopo kwa wafanya biashara watakao hitaji na kutakuwa na utaratibu ili kupunguza gharama za ukopeshwaji Wajane wote watakopeshwa bila riba fedha watakazopata ndizo watakazorudisha
Mh Mavunde
Soko la Mavunde linagharimu takribani milioni kumi na tisa katika ukarabati na Ofisi ya jiji imetenga fedha kwaajili ya ukarabati wa masoko ikiwemo soko la Mavunde.
0 Comments