WAANDISHI WA HABARI SHIRIKIANENI NA JESHI LA POLISI -MISIME

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

MSEMAJI wa Jeshi la polisi Tanzania SACP David Misime ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kukuza maslahi mapana ya taifa pale wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Misime ametoa kauli hiyo leo Septemba 19,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua mdahalo wa kitaifa kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari ulioandaliwa na Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), kauli mbiu ikiwa "Shambulio lolote kwa mwandishi wa habari ni shambulio kwa Umma".

Akifungua mdahalo huo Misime amesema kuwa kazi kubwa ya Jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zake lakini pia kuhakikisha usalama wa polisi, waandishi pamoja na jamii kwa ujumla wanakuwa salama kabisa.

Kazi ya waandishi wa habari ni muhimu sana na wakishirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa sahihi zenye kulinda amani ya nchi pamoja na kulinda maslahi mapana ya nchi ni wazi kila mmoja atakuwa salama zaidi hapatakuwepo na malalamiko

Waandishi mnatakiwa kuandika habari ambazo zitakuwa na uwezo wa kulifanya taifa kuwa na sifa ya kuwavutia wawekezaji kuingia nchini bila kuwa na shaka yoyote jambo ambalo litafanya nchi kuwa katika hali ya utulivu

Misime.

Pamoja na mambo mengine Misime amesema kuwa waandishi wakishirikiana vyema na jeshi la polisi hata kwa kufichua au kutoa taarifa sahihi ni wazi polisi atakuwa salama na wananchi kwa ujumla wake.

Naye Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya ambaye amesema kuwa ni wajibu wa mwandishi wa habari kufanya kazi yake kwenye mazingira rafiki bila kubughudhiwa.

Simbaya ametoa kauli hiyo muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi abaye alifungua mdahalo huo, na kueleza kuwa kama mwandishi atakuwa anafanya kazi kwa kunyimwa uhuru itapelekea watanzania kukosa habari na mwandishi mwenyewe kushindwa kutimiza wajibu wake.

Aidha amesema kuwa mwandishi wa habari anatakiwa kufanya kazi kwa kupewa uhuru na kulindwa anapokuwa katika mazingira rafiki kwa lengo la kutimiza majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya taifa.

Naamini Mdahalo huu utasaidia kutengeneza msingi mzuri kwa waandishi wa habari katika kutimiza majukumu yao ya kila siku kwa uhuru na kuzingatia maslahi mapana ya taifa

Simbaya

Kwa upande wake Dkt. Rose Reuben Mkurugenzi Mkuu wa TAMWA amesema asilimia 64 ya Wanawake waliopo katika vyumba vya habari vya Jiji la Dar es Salaama wamefanyiwa unyanyasaji wa Kingono ikiwemo Rushwa ya ngono na sababu kubwa ili kazi zao ziweze kutoka katika vyombo vya habari na wengine ili wapate kazi za nje ya Mkoa.

Ameongeza kuwa Wanawake wengine wamejikuta wakiingia katika ukatili wa kingono katika vyumba vyao vya habari kutokana na kuhofia kupoteza kazi zao.

Kukosa kujiamini kwa Wanawake katika vyumba vya habari na kushindwa kuelezea madhila wanayokumbana nayo katika kazi zao imeendelea kuleta ugumu katika kupambana na matukio ya ukatili ama Rushwa ya ngono

Na kuongeza kuwa ni 

Vyema kutoa taarifa ya matukio kama haya ili kutoa nafasi ya kushughulikiwa Wanawake msikae kimya wala kuyafumbia macho maana athari ni kubwa na wale walioamua kukubaliana na aina hiyo ya Rushwa ya ngono wanapata manyanyaso sana huku wengine walioamua kuacha kazi ya uandishi wa habari ambayo kimsingi ndio taaluma zao jambo ambalo linawakosesha haki ya kufanya kazi zao

Dkt.Rose

Mdahalo huu wa kitaifa umehusisha waandishi wa habari kutoka katika Klabu za mikoa tofauti tofauti nchini, Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jeshi la Polisi na wadau wengine wa habari lengo likiwa ni kuboresha masuala mazima ya Ulinzi na Usalama kwa waandishi wa habari



Post a Comment

0 Comments