SERIKALI Kupitia
Wizara ya Afya kwa
kushirikiana na Ofisi
ya Rais Tawala
za Mikoa na
Serikali za Mitaa
[TAMISEMI] na Wadau mbalimbali
imesema inatekeleza afua
mbalimbali kwa ajili ya kuwakinga kudhibiti
na kukabiliana na magonjwa hususani kuwakinga
watoto na magonjwa
yanayozuilika na chanjo .
Hayo yamesemwa
na Waziri wa
Afya Mhe Ummy
Mwalimu alipokua akizungumza
na vyombo vya
habari Septemba 8, mwaka 2023
Jijini Dodoma na
kubainisha magonjwa yanayozuilika
kwa chanjo ni Polio,
Surua, Saratani ya mlango wa
kizazi, kifaduro, kuhara kukali,
kichomi na kifua Kikuu.
Pia amesema
kwa kipindi cha
miaka mitatu mfululizo nchi yetu
kama ilivyo mataifa
mengine ilikabiliana na
janga la ugonjwa
wa UVIKO -19 ambao
umeleta athari kadhaa
kwa afua zingine
za afya ikiwemo kuathiri
mwitikio wa chanjo mbalimbali
nchini.
Tumefanya tathimini kuanzia mwaka 2020-2022 tumeona kuna watoto 1,988,022 hawakupata chanjo yoyote vilevile kwa kipindi hicho [2020-2022] jumla ya watoto 1,595,564 hawakukamilisha ratiba za chanjo zote na hivyo kupelekea kujitokeza kwa visa na milipuko ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambayo yalikua yamedhibitiwa ikiwemo ugonjwa wa Surua, Rubella na Polio
Ummy.
Aidha amesema
kupitia ukaribu wa kijiografia
na mwingiliano mkubwa
wa watu uliopo
kati ya nchi
yetu na nchi
zenye mlipuko wa
ugonjwa wa Polio
hivi sasa, anapenda kuutarifu
umma kuwa kutakua
na Kampeni maalumu
ya utoaji wa chanjo ya
matone dhidi ya
Polio [nOPV2] kwa watoto wote
wenye umri chini
ya miaka [8] kampeni hii
itafanyika kwa siku
nne kuanzia tarehe
21 – 24 Septemba, mwaka 2023
katika mikoa sita
inayopakana na nchi
zenye mlipuko wa
Polio ambayo ni
Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi ,Songwe na Mbeya.
Natumia fursa hii kutoa maelekezo kwa waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Tanzania Bara zitakazohusika na zoezi hili kusimamia kwa karibu maandalizi na utekelezaji wa Kampeni hii kupitia Kamati za Afya ya Msingi ngazi za Mikoa na Wilaya. Aidha nawaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha upatikanaji wa chanjo
Ummy
0 Comments