MAMLAKA ya
Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na Watanzania wote kwa ujumla
kuwa makini na matapeli wanaotumia mitandao kwa kutumia jina la TRA kufanya
uharifu.
Hayo yamesemwa leo Septemba 15 na Meneja wa TRA Mkoa wa kikodi Dodoma Castro John wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kampeni ya zoezi la (TUWAJIBIKE) ambalo linahusisha uwajibikaji wa utoaji risiti.
Tumekuwa tukipata kesi nyingi sana kuhusiana na hao matapeli mitandaoni na hizo changamoto tutahakikisha tunazitatua kwa haraka kwa kuendelea kutoa elimu kwa wafanya biashara na wananchi wote kwa ujumla,
Lakini pia kuweka nguvu kwa kundi la Wanunuzi ili kuhakikisha suala hili la matapeli mitandaoni linapungua kwa uharaka mkubwa
Castro
Kadhalika Castro amesema kwa wale wanaofanya biashara mitandaoni wahakikishe wanatoa risiti kwasababu wapo wafuatiliaji wanafuatilia masuala yote ya biashara mitandaoni hivyo atakayebainika anaenda kinyume, sheria itafata mkondo wake.
Naye moja kati ya wafanyabiashara waliotembelewa na TRA Lupi Mwaikambo ambaye anajishughulisha na uuzaji wa vifaa vya nyumbani ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kampeni ya tuwajibike huku akiitaka iendelee kutoa elimu zaidi kwa jamii.
TRA elimu hii itolewe kwa wananchi mara kwa mara kwa kuwa ni kitu ambacho kinaonekana hakifahamiki kwenye jamii, elimu ya kudai risiti kwa wananchi haipo kwahiyo endapo elimu hii ikatolewa mara kwa mara jamii itafahamu umuhimu wake
Binafsi mimi mteja akisahau risiti namuita kabisa kwahiyo natoa rai kwa jamii na wafanyabiashara wenzangu watumie mashine hizi za EFDS kwanza ukifanya hivyo ukakidhi vigezo utafanya biashara yako katika mazingira ya amani bila bugudha
Lupi
0 Comments