TIMU ya taifa ya Tanzania Taifa Stars
imefanikiwa kufuzu AFCON kwa mara ya tatu katika historia baada ya kutoa sare
ya 0-0 na timu ya taifa ya Algeria katika dimba la Stade du 19 Mai 1956 Annaba
na kuwawezesha mashujaa hao wa mama Samia kutinga moja kwa moja katika michuano
ya Afica Cup Of Nation ijulikanayo kama AFCON.
Mchezo huo ulipamba moto kwa dakika 95
huku ukiamuliwa na muamuzi mwenye umri wa miaka 37 ajulikanae kwa majina ya
Djindo Louis Hougnandande raia wa Benin aliyesimama kama hakimu wa kesi hiyo na
akitokwa na jasho jingi baada ya kukamilisha mikimbio ya wachezaji wa Algeria
waliokuwa wanapiga pasi nyingi na kushtukizwa na mashambulizi ya ghafla kutoka
kwa timu ya Tanzania Taifa Stars.
Kocha wa timu ya Taifa Stars Adel
Amrouche amesema waliwaheshimu sana wapinzani wao pamoja na mechi na ndiyo
sababu ya timu kupata matokeo mazuri katika mchezo muhimu na wa historia ya
Taifa kwa ujumla.
Mechi ilikuwa ya kasi kwani mchezo wa mara
ya mwisho kwa timu hizo kukutana mnamo tarehe 8 Juni mwaka 2022 Algeria aliweza
kumfunga Tanzaniza goli 2-0 katika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini
Da-Es-Salaam wenye idadi ya kuingiza takribani mashabiki 60,000 walipata
ushindi kwa kuwachapa waenyeji wao kwa magoli pekee yaliyowekwa kambani na Ramy
Bensebaïni mnamo dakika ya 45 pamoja na Mohamed Amoura akipokea pasi maridadi
kutoka kwa Ismael Bannacer mnamo dakika ya 89 ya mchezo.
Katika mchezo huo timu ya Taifa Stars
walijitahidi kupambana kadri ya uwezo wao bila mafanikio hali iliyosababisha
vijana hao waliokuwa wakinolewa na Kim Poulsen kushindwa kutumia uwanja wa
nyumbani vizuri na kuambulia kichapo kilicho waacha hoi mashabiki wa timu hiyo.
Ingawa katika mchezo wa marudiano timu
ya Taifa Stars walipambana bila mafanikio ya kupata goli la ugenini dhidi ya
Algeria kwa lengo la kulinda nafasi ya pointi moja iliyowatenganisha na
mahasimu wao kutoka Afrika mashariki Uganda The Cranes ambayo imeshika nafasi ya
tatu katika kundi F ikitamba kwa mabao mawili dhidi ya Niger katika uwanja wa
Stade de Marrakech na haikuweza kuwafanya Taifa Stars kupaniki na kuleta shida
yeyote hadi dakika 90 za mchezo huo kukamilika.
Mashabiki wa timu ya Taifa Stars wamesema wanashukuru Mungu kwa nafasi ya historia ya kutinga katika michuano ya AFCON na wapo tayari kwa timu yeyote itakayokatiza mbele yao huku wakijinadi kuwa uwanja wao wa nyumbani ni maarufu kwa kuzifunga timu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.
Michuano ya Afica Cup Of Nations AFCON itaungurumishwa nchini Ivory Coast kuanzia tareh 13 Januari hadi tareh 11 Februari 2024 ikihusisha jumla ya mataifa 24 yaliyofuzu michuano hiyo na kabumbu itasakatwa katika viwanja sita bora ambavyo vinapatikana ndani ya miji mitano nchini Ivory Coast.
0 Comments