WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mh Angellah Kairuki amesema Tanzania imeshinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa kongresi ya 50 ya shirikisho la vyama vya wafuga Nyuki Duniani ( APIMONDIA) inayotarajiwa kufanyika Septemba 20 hadi 25, 2027 Jiji Arusha.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongresi ya 50 ya shirikisho la vyama vya wafuga Nyuki Duniani (APIMONDIA) mwaka 2027.
Ushindi huu ni muhimu kwa Tanzania na Bara la Afrika utatukutanisha na wadau wa sekta ya Nyuki Duniani wakiwemo wafugaji wa Nyuki, wafanyabiashara, wasafirishaji, wazalishaji wa mazao ya Nyuki watumiaji wa bidhaa na huduma kama vile Utalii wa nyuki, uchavushaji mazao huduma za matibabu ya Nyuki watafiti na wanasayansi, wanafunzi, viongozi wa serikali na watoa huduma mbalimbali
Kairuki
Waziri Kairuki amesema wito Kwa wadau wa ufugaji Nyuki na Taasisi mbalimbali zinazohusika na ufugaji nyuki zitumie fursa vizuri kuongeza tija katika ufugaji na Biashara nzima ya mazao ya Nyuki kuongeza wigo mashirikianao na Taasisi mbalimbali na kuvutia uwekezaji katika sekta hio.
Kongresi hii ya 50 APIMONDIA ni fursa ya kubadilisha ujuzi wa uvumbuzi na ushirikiano katika sekta ya ufugaji wa Nyuki ambapo utajumuisha midahalo ya kisayansi katika ufugaji wa Nyuki kujua maendeleo ya ufugaji wa nyuki uzalishaji asali pamoja na uchavushaji mashindano ya ubunifu katika ufugaji Nyuki
Kairuki.
Mkutano huu unakadiriwa kushirikisha wadau zaidi ya 600 toka mataifa mbalimbali duniani hivyo Tanzania tutanufaika katika kuchochea ukuaji wa sekta ya Nyuki na uhifadhi, kuongeza mchango wa sekta katika pato la taifa, kuchochea utalii nchini na kuvutia wawekezaji wa viwanda na teknolojia katika sekta ya ufugaji.
Watanzania watambue Ushindi huu unakwenda kufanya nchi ya Tanzania ya pili barani Afrika kupewa jukumu la kuandaa mkutano huo tangu kuanzishwa kwa APIMONDIA miaka takribani 130 iliyopita Afrika kusini ndio nchi iliyotangulia .
APMONDIA ni shirikisho la umoja wa vyama vya wafuga nyuki duniani lililoanzishwa mwaka 1895 na makao makuu yake ni Roma nchini Italia ambapo Tanzania ilijiunga mwaka 1984
0 Comments