SERIKALI imezitaka Taasisi zote za manunuzi
kuhakikisha zinafanya ununuzi wa umma kupitia mfumo wa ununuzi wa
kielektroniki NeST kuanzia tarehe 1 Oktoba mwaka 2023 ili kuziba
mianya ya Rushwa kwenye ununuzi wa umma.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Mh. Hamad Chande wakati wa kukabidhi ripoti ya tathimini ya utendaji kwa mwaka wa fedha 2022/23 Septemba 29, 2023 Jijini Dodoma.
Mh.Chande amezikumbusha Taasisi nunuzi zote za serikali kuzingatia waraka wa hazina na 2 wa mwaka 2023/24
Naagiza hatua kali zichukuliwe kwa wote watakaokiuka maelekezo haya, Katibu Mkuu Hazina na Mlipaji mkuu wa serikali nakuelekeza kuwa hili ulisimamie na kulifuatilia kwa karibu mno
Chande
Aidha Naibu Waziri amebainisha kulingana na uchunguzi na ukaguzi uliofanywa na Mamlaka ya ununuzi PPRA serikali imepata hasara ya jumla ya TZS 8.77 billion kutokana na ukosefu wa uwajibikaji, ufanisi, uwazi na uadilifu kwenye Taasisi 12 zilizochunguzwa.
Natoa maelekezo kwa vyombo husika vya jinai ikiwemo TAKUKURU kuchukua hatua stahiki aidha ni dhahiri kuwa serikali haitazivumilia hata kidogo Taasisi zinazokiuka sheria
Chande
0 Comments