MJUMBE wa bodi ya Singida Fountain Gate ambaye pia ni Mbunge wa Makete Festo Sanga amesema timu hiyo ina malengo ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu na kufika hatua ya makundi na hata nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Sanga ameyasema hayo alipozungumza na CPC BLOG Jijini Dodoma na kubainisha kuwa mechi mbili walizofungwa Singida Fountain Gate zimewafanya washituke mapema na kuamua kumleta kocha Ernest Middendorp kutoka nchini Ujerumani
Tumefanya kikao na wachezaji pia tumefanya maamuzi ya kubadilisha kocha (Hans van de Pluijm) na kuleta kocha mpya ambaye ana historia kubwa kwenye soka la Afrika na sisi kama timu tuna malengo, tumechoka kuona ubingwa unabaki Dar es salaam sasa ni wakati wa mikoani, ni matamaini yetu kuona ubingwa unakuja Singida
Sanga
Aidha ameendelea kwa kusema niwaambie watanzania wasikatishwe tamaa na yale matokeo tuliyopata dhidi ya JKU na tumewapa uangalizi wachezaji.
Mishahara na stahiki wanazozipata zina hadhi kubwa mchezaji mmoja wa Singida Fountain Gate mshahara wake anaolipwa unalingana na wachezaji wote wa JKU lazima waonyeshe heshima kwa kile wanachopata
Sanga
Sanga pia amewaomba mashabiki wa soka nchini kuendelea kuisapoti timu ya Taifa Taifa stars na kuacha kutoa maneno yasiyofaa mitandaoni kutokana na kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kwa baadhi ya mastaa kama Shomari Kapombe na Mohamed Hussein Shabalala kwani timu ya Taifa haijengwi na wachezaji wachache bali timu ya Taifa inajengwa na wachezaji wengi hivyo anawaomba watanzania waendelee kuisapoti timu yao
Timu ya Taifa inajengwa na wachezaji wengi kutoitwa leo haimaanishi wewe sio bora mfano Kevin John ameachwa tuna amini sio kwamba siku zote ataachwa inawezekana timu inampa chachu timu ya Taifa ina wachezaji 11 haiwezekani kila siku acheze mtu mmoja
0 Comments