SIMBACHAWENE: e-GA NA TAASISI ZA SERIKALI SHIRIKIANENI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UNUNUZI WA MIFUMO.

                                   

📌RHODA SIMBA

SERIKALI imetoa rai kwa Taasisi za Serikali kushirikiana na kituo cha Utafiti, Ubunifu na uendelezaji wa mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA badala yakuendelea kununua mifumo ambayo inatumia fedha nyingi.

Rai hiyo imetolewa leo Septemba 18 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha Utafiti, Ubunifu na uendelezaji mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGa) kilichopo Chuo Kikuu cha Dodoma ndaki ya CIVE.

Simbachawene amebainisha kuwa ni vyema sasa eGA wajenge mifumo mbalimbali kulingana na ukuaji wa teknolojia ili kupunguza gharama kubwa za ununuzi wa mifumo kutoka nje ya nchi.

Mara nyingi tunaposoma tunakimbilia kuajiriwa, nafikiri tukafikiri zaidi kujiajiri , mifumo kama hii ya e- mrejesho, e- Mkutano tunaijenga si kazi ndogo lakini kama serikali tunainunua kwa gharama kubwa kwa kipindi kirefu sana na mpaka sasa bado zipo Taasisi za serikali ambazo zinanunua mifumo wakati sisi taasisi yetu hii ya e- GA inabuni na kujenga mifumo mbalimbali 

Aidha amewataka wananchi kuendelea kutumia mfumo wa e- Mrejesho ili kurahisisha mawasiliano naserikali yao.

Niseme tu kwamba pamoja na kwamba mmetegeneza lakini mmetoa mifumo mbalimbali ambayo imetegenezwa nainayotatua changamoto zetu badala yakutegemea mifumo ya nchi za nje kama vile mfumo wa e- Mkutano ambao mmeusema lakini pia mfumo wa e- Mrejesho unawezesha wananchi kuwasiliana na serikali pamoja na kiwasilisha kero zao na malalamiko yao lakini maoni , pongezi kwakweli huu ni mfumo ambao umetusaidia sana

Mbali na hayo Simbachawene amesema uanzishwaji wa kituo cha Utafiti na Ubunifu ni moja ya Jitihada za Serikali kujikita katika kuwa na mazingira ya kufanya utafiti wa kutosha kwenye eneo la TEHAMA lakini pia kufanya majaribio ya vitendo vya bunifu zinazovumbuliwa na kukuza vipaji kwa vijana wabunifu na wenye vipaji vya TEHAMA na mwisho kuwa na watalaamu wabobezi katika nyanja ya TEHAMA.

Mamlaka ya Serikali Mtandao inatekeleza programu ya kukuza bunifu kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Programu hii imefanyika kwa misimu mitano mfululizo kuanzia Mwaka 2019 hadi sasa 2023

Serikali Mtandao wanafanikisha azma hii kwa kushirikiana na vyuo vikuu vinavyotoa mafunzo ya TEHAMA. Hivyo basi program hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa"amesema Simbachawene 

Amesema juhudi za Serikali kujiimarisha kwenye eneo la TEHAMA ni za kipaumbele na hivyo jitihada za kuboresha Utafiti na Ubunifu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwa na mazingira ya kuweza kuchukua vijana wengi zaidi wenye vipaji na wabunifu kwenye eneo la TEHAMA kuweza kufanya majaribio na kujiendeleza kwa vitendo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya serikali Mtandao e-GA Mhandisi Benedict Ndomba amesema pamoja na mafanikoo mengi yaliyoppatikana katika mamlaka hiyo lakini bado kuna changamoto kubwa ya ufinyu wa eneo na fedha kwaajili ya mazoezi hivyo kama mamlaka imejipanga kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali .

Hata hivyo amesema kuwa Serikali mtandao ina majukumu mbalimbali ikiwemo ya jitihada za Serikali kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya TEHAMA.

Kadhalika amesema kuwa kupitia ubunifu, utafiti na mazoezi kwenye maeneo hayo kama nchi inakuwa katika nafasi nzuri ya kushindana kwenye uchumi wa kidigitali na nchi zingine.



 

Post a Comment

0 Comments