SERIKALI YATOA UFADHILI WA MASOMO KWA WATUMISHI 500

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

SERIKALI kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza 2023/24 umetoa ufadhili masomo ya muda mrefu na muda mfupi nje ya nchi kwa watumishi 500.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknoljia ya Habari Mohammed Khamis Abdullah, alisema hayo jana jijini hapa wakati wa hafla ya kutoa vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia mradi huo.

Abdullah, alisema katika ufadhili huo watumishi 50 ndiyo watakaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya masomo ya muda mrefu na wengine 450 ni masomo ya muda mfupi.

Niwapongeze sana nyie ambao mmekuwa katika awamu hii ya kwanza ambao idadi yenu mpo 20 kati ya watu 211 waliomba nafasi za kushiriki mafunzo haya.

Niwasihi huko mtakapo kwenda kitu cha kwanza ni kutanguliza uzalendo wa taifa lenu na mtakachojifunza kule lazima mkilete nchini ili kuongeza tija katika masuala ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano

Alisema ufadhili huo ni matokeo ya dhana ya serikali ya awamu ya sita kukuza na kuimarisha rasilimali watu ili taifa kwenda katika dunia ya kidijitali.

Zamani tulikuwa serikalini tunatumia makaratasi lakini hivi sasa kuna kitu kinaitwa serikali mtandao hivyo basi muende na mtakacho jifunza mhakikishe kinakuja kulinufaisha taifa na ujuzi huo mkawafundishe na wenzenu

Kadhalika, alisema kupitia mradi wa Tanzania ya kidijitali serikali imepanga kujenga vyuo viwili vya TEHAMA katika mkoa wa Dodoma na Kigoma pamoja na vituo nane vya ubunifu.

Lakini pia tunapanga kuwa na sera mpya ya TEHAMA na Ubunifu ili kuzikuza na kuzisimamia bunifu zote hivyo mkajifunze na mnaweza kuwa hata wakufunzi katika vyuo vyetu vya TEHAMA ambavyo tumepanga kuvijenga

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Gerald Mbwafu, aliwataka watumishi hao waliopata nafasi ya masomo nje ya nchi kuzingatai sheria za nchi na vyuo wanavyokwenda kusoma.

Masuala ya kuzingatia ni mengi sana ambayo yamekuwa yakitufanya baadhi ya watu wetu kurudisha nchini jambo la kwanza linalotuathiri sana ni kuheshimu taratibu za kule tunakokwenda ambazo ni tofauti na za Tanzania.

Pia nawata mkajiepushe na mashtaka ya madai na jinai wizi na utapeli havivumiliki kabisa lakini pia matumizi ya dawa za kulevya ukibainika ni kifungo au kukurudisha nchini na kulitia aibu taifa

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Mrope, alisema serikali itahitaji kuwatumia watumishi hao kwa manufaa ya Taifa.

Tunataka mnaporudi nchini mara baada ya mafunzo yenu tuwatumie vizuri, tunashida sana zinapotoka nafasi za mashirika ya kimataifa kama nchi tunakosa watu wenye sifa lakini nyinyi mkirudi mtasaidia kupunguza changamoto hiyo hivyo mkirudi mje na haiba ileile na siyo mje na haiba ya ulaya



Post a Comment

0 Comments