KATIBU mkuu wa wizara ya habari mawasiliano na
technolojia ya habari Mohamed Khamis Abdulla ameyasema hayo katika hafla ya
kuwaaga watumishi 20 kati ya 211 wanaokwenda kusoma nje ya nchi na kurudi
kuhudumu ndani ya serekali iliyofanyika tarehe katika ukumbi wa Rafiki Hotel
jijini Dodoma.
Akizungumza na
wanahabari katibu mkuu wa wizara ya habari mawasiliano na technolojia ya
habariMohamed Khamis Abdulla alisema anapenda kumshukuru Mola kwakuwezesha leo
hii kuwa pamoja katika hafla hii muhimu ya kuwaaga, kuwapa nasaha na utiaji
saini wa mikataba ya kuhakikisha watumishi ishirini (20) wanaokwenda kusoma nje
ya nchi na kurudi kuhudumu ndani ya serikali.
Alisema anapenda
kutoa pongezi za dhati kwa watumishi hao kwa kubahatika kupata nafasi hiyo ambayo
ina watumishi wengi walioomba na kwa kutambua umuhimu wao wa kujiendeleza
kimasomo katika ngazi ya uzamili wa taaluma mbalimbali zinazoibukia kwenye
masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano na ufadhili huu walioupata ni
kupitia mradi wa Tanzania ya kidijitali.
Mradi wa Tanzania ya kidijitali unalenga kuleta mabadiliko ya kidijitali kwa kuwezesha maunganisho ya kijiditali ya kikanda na kimataifa ili kuweza kukuza uchumi wa kidijitali kuongeza na kubuni ajira zitakazotokana na ubunifu na uwepo wa mazingira wezeshi na ukuzaji wa viwanda vidogo vidogo.
Katika mradi huu ni muhimu kwaajili ya kukuza uchumi wa viwanda na ustadi wa wa TEHAMA nchini na jambo la muhimu kwenu ni kuhakikisha mnarudi mkiwa na uelewa wa Teknolojia zinazoibuka yaani “emerging Technology'
Abdulla.
Pia naibu katibu
mkuu ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Xavier Mrope
Daudi alitoa ushauri kwa watumishi wanaokwenda kusoma nje ya nchi kupitia mradi
huo wa kidijitali kwa awamu ya kwanza ya mwaka 2023/2024 kuwa matarajio yake
wataenda kushika elimu na kuweka jitihada katika masomo yao pamoja na
kuzingatia haiba watakapokuwa katika maandhari ya kigeni.
Naibu katibu
mkuu aliongezea kwa kusema kuwa uchumi wa kidijitali ni muhimu sana kwa
serikali kwani ni chanzo cha vipaji na serilaki ya awamu ya sita moja ya
kipaumbele ni kukuza vipaji ndio maana imetengwa bajeti ya shilingi bilioni 5.4
ambayo itasaidia kujenga miradi kadhaa ikiwemo vyuo viwili mkoani Dodoma na
Kigoma pia vituo nane vya ubunifu vinategemea kuanza kujengwa.
Katibu mkuu
alimalizia na kusema chanzo pekee cha ujuzi ni uzoefu na kwa kuzingatia hili
ninawatakia watumishi wetu hawa 20 kila la kheri na wawe na mafanikio kwenye safari
yao ya kupata uzoefu mpya katika kutafuta maarifa ili waweze kuwa na
weledi na waweze kuleta mchango mkubwa kwenye safari hii ya uchumi wa
kidijitali ambapo sekta zote za kiuchumi zinategemea TEHAMA.
0 Comments