SERIKALI KUSHIRIKIANA NA LAKE GESI KUTOKOMEZA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA

📌SUZANA ALEX 

IKIWA ni kampeni ya kumtua mama Kuni kichwani, Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya  Lake Gesi imetoa jumla ya mitungi 13,500 katika Mikoa mitano  ambayo ni Dodoma, Arusha, Mwanza, Geita na Morogoro ili  kuondokana na  matumizi ya kuni na mkaa  kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

Akizungumza kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora ambaye pia ni mbunge  wa Jimbo la Kibakwe George Simbachawene amesama matumizi ya nishati ya gesi yatasaidia katika utunzaji wa mazingira.

Simbachawene amesema, uamuzi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kutoa zawadi Kwa watanzania wachache hao watakaopata kupitia kwa wabunge ni uamuzi mzuri ambao utachochea utunzaji wa mazingira

Naye aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amesema

Tunakoelekea ni kwenye kuhifadhi mazingira na kupambana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi na sasa msisitizo ni kwa akina mama na kina baba sasa itumike Gesi badala ya kuni na mkaa

Job Ndugai.

Kwa upande wake meneja masoko wa Lake Gesi Matina Nkulu amesema wao  kwa kushirikiana na wakala wa nishati Rea itawarahisishia akina mama kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Tutafanya kampeni ya kuwaelimisha wananchi jinsi ya kutumia mitungii hii na wapi watapata Gesi iliyobora. Serikali imejidhatiti leo ni siku ya kwanza na ni siku 

 

Post a Comment

0 Comments