SERIKALI KUPITIA WIZRA YA AFYA KUTOA CHANJO YA POLIO KWA MIKOA SITA NCHINI

 ðŸ“ŒAISHA SULEIYMAN

WIZARA ya Afya itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadau mbalimbali katika kutekeleza afua za kukinga, kudhibiti na kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayozuilika kwa chanjo nchini. 

Hayo yamesemwa  leo Septemba 8 jijini Dodoma na Waziri wa afya Mh Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wanahabari  kuhusu kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio kwa watoto.

Ameleza kuwa Wizara imekuwa ikifuatilia mwenendo wa magonjwa haya, kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara na kusisitiza hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kukinga, kudhibiti na kukabiliana na magonjwa hayo. 

Maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Polio yametolewa taarifa katika nchi zinazopakana nasi mfano Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia. Hali hii inaongeza tishio na hatari ya maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Polio kwa nchi yetu hususani katika Mikoa inayopakana moja kwa moja na nchi 

Mwalimu 

Aidha piya ameleeza kuwa watoto tisa kati ya kumi wenye maambukizi ya ugonjwa wa Polio huwa hawaonyeshi dalili. Vilevile mmoja kati ya watoto mia mbili wenye maambukizi hupata ulemavu wa kudumu. Ameongeza kwa kusema kwa mara ya mwisho mgonjwa wa Polio nchini aligundulika mwaka 1996. Hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitangaza Tanzania kuwa nchi isiyo na maambukizi ya ugonjwa wa Polio mnamo mwezi Novemba, 2015. 

Ameendelea kwa kusema mnamo tarehe 26 Mei, 2023, Wizara ilipokea taarifa za uwepo wa mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja ambaye alionyesha dalili za kupooza kwa ghafla. Mtoto huyo alitolewa taarifa kutoka Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa. Uchunguzi wa Maabara ulithibitisha kuwa mtoto huyu ana maambukizi ya virusi vya polio 

Kufanikisha Kampeni hii, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wadau wa chanjo imeshafanya maandalizi kwa ajili ya kuwezesha zoezi hili kuendeshwa bila kuathiri shughuli zingine za wananchi. Aidha, wakati wa Kampeni kutakuwa na jumla ya timu yenye jumla ya watoa huduma za afya 5,291 kwa Mikoa yote sita (6) itakayofikiwa na zoezi hili ambapo kila timu itakuwa na watoa huduma watatu. Timu hizi zitakuwa zinatoa huduma ya chanjo kwa walengwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya, nyumba kwa nyumba, shuleni na maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ikiwemo nyumba za Ibada.

 

Post a Comment

0 Comments