WAZIRI wa Madini Antony Mavunde amesema
serikali itaijengea uwezo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania
(GST) ili kuongeza ufanisi kwasababu ndio moyo wa Madini.
Ameyasema hayo Septemba 11, 2023 Jijini Dodoma alipokua akizungumza na wachimbaji wadogo na kubainisha hatofumbia macho wanaokiuka sheria na kuhakikisha anazuia utoroshaji ili nchi inufaike na Madini.
GST ndio moyo wa Madini hapa Tanzania hatuwezi kuendelea bila GST nakwenda kuijengea uwezo iwe Taasisi imara, Taasisi kiongozi ambayo itatoa taarifa muhimu za kijiolojia ili kuweza kusaidia kufikia malengo yetu
Mavunde.
Ninyi leo hapa mna changamoto kubwa kwasababu hamna taarifa ya maeneo yetu, wachimbaji wa Nchi hii wanachimba kwa kubahatisha na ndio maana kuna wakati wapo wanaohisi biashara hii kuna majini, hakuna njia fupi Madini ni Sayansi tukipiga picha nchi nzima tukawa na taarifa sote tutafanikiwa
Mavunde
Naye Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) John Bina amesema Chama hicho kilianza mwaka 1986 ikiwa na lengo la kuwaunganisha wachimbaji wadogo na kukuza soko ndani na nje ya nchi na naipongeza STAMICO kwa kuwajali wachimbaji wadogo.
FEMATA tunaendelea kupaza sauti kwa niaba ya wachimbaji wadogo ili Tume ya Madini waweze kutenga maeneo kwaajili ya wachimbaji wadogo
Bina
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa kati Tanzania TAMIDA amesema azma yao ni kuhakikisha Madini yanaongezeka thamani Tanzania
Naye Mwenyekiti wa Chama cha mabroker CHAMATA Jeremiah Simioni ameiomba serikali iangalie jambo la leseni na pia minada ya Madini ianzishwe mapema.
0 Comments