RAIS wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano Maalum
wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia, ufunguzi huu umefanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar
es Salaam jana 11 Septemba, 2023.
Akifungua Mkutano huo Rais Samia, amesema lengo ni kutathimini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi na Hali ya siasa Nchini, pia amezungumzia mambo mbalimbali juu ya mustakabali wa Taifa letu.
Katika Mkutano huo, Viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwepo Viongozi wa Kiserikali, Viongozi wa Kisiasa, Mabalozi, Viongozi wa Dini na Wadau mbalimbali.
Aidha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika ufunguzi huo imewakilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Jumanne Sagini (Mb) ambaye ameambatana na Katibu Mkuu Kaspar Kaspar Mmuya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Maduhu Kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Kiserikali, Viongozi wa Kisiasa, Mabalozi, Viongozi wa Dini na Wadau mbalimbali wakati wa ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ambao umeanza leo Septemba 11 - 13, 2023.
0 Comments