ASASI
za kiraia zimekutanaa jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa Mpango mkakati wa
Jumuiya na Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao unazitaka nchini wanachama
kuwa na uchumi wa kati wa viwanda na amani ili kuwa na maendelevu ifikapo 2050.
Mkurugenzi wa Shirika la ActionAid Tanzania
Bavon Christopher, alisema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye
kikao cha siku tatu cha kujadili ambavyo Tanzania imefanikiwa kuutumia Mpango
mkakati wa SADC, kwenye mipango yake ya ndani.
Bavon, alisema lengo la kikao hicho ni kutathimini ni kwa namna gani Tanzania imeweza kuuweka Mpango mkakati huo kwenye mipango yake ya ndani.
Mpango mkakati huu ni wa miaka 10 kuanzania 2020 hadi 2030 ambao umejikita kwenye kuboresha viwanda, kilimo, miundombinu, haki za binadamu, mapambano dhidi ya mabadiliko tabianchi na mambo mengine
Amesema kikao hicho pia kimejumuisha wadau kutoka Asasi mbalimbali za kiraia pamoja na wawakilishi wa serikali kutoka wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wabunge wa SADC.
Maono ya Jumuiya ya SADC, ni kuona nchi wanachama zinakuwa na uchumi wa kati wa viwanda na amani inadumishwa ili kuwa na maendeleo kwa wananchi ifikao 2050 sasa lengo la kukutana hapa ni kuona ni kwa jinsi gani yale ambayo tulijipangia kuyatekeleza sisi kama Asasi tumeyafanikisha kwa kiwango gani.
Lakini pia serikali yetu imetekeleza kwa kiasi gani kuufanya Mpango mkakati huu wa SADC kuwa sehemu ya mipango yake ya ndani ambayo itatekeleza lakini pia kazi yetu sisi ni kuisimamia serikali, kuishauri na kutoa msaada wowote inaouhitaji ili kufanykisha utekelezai wake
Bavon
Aidha, amesema kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya nyuma ambavyo vilitumika kwa ajili ya Asasi za kiraia pamoja na serikali kujiwekea malengo ya utekelezaji wa Mpango mkakati huo.
Kikao cha kwanza tulikaa mwaka 2021cha pili 2022 na kichi leo ni cha tatu ambapo tunaagalia ni kwa kiasi gani tumetekeleza lakini ni mambo gani yanapaswa kufanywa kuanzia leo hii hadi hapo tutakapo kutana tena Septemba mwaka 2024 vivyohivyo kwa serikali pia kueleza nini imefanya na nini watafanya kuanzia leo hii hadi mwakani tutakapo kutana tena
Hata hivyo, ameipongeza serikali ya Tanazani kwa namna ambavyo inaendelea kushiriki katika Jumuiya hiyo ya SADC, hali ambayo itasaidia taifa kupiga hatua kiuchumi.
Niwapongeze sana viongozi waliotangulia akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye aliona upo umuhimu wa sisi kama taifa kushirikiana na mataifa mengine katika jumuiya kwani sisi Afrika hatuwezi kupiga hatua kama hatutakuwa wamoja umoja ndiyo siri ya mafanikio yetu.
Leo hii tunapoondoa vikwazo katika mataifa mengine tunaruhusu usafirishaji wa bidhaa zetu kutoka nje na zingine kuingia ili kuimarisha uchumi wetu na bara letu kwa ujumla
Daines Mtei kutoa Wizara ya Kilimo alisema kuwa kikao hicho umetia fursa kwa seriklai pamoja na Asasi za kiraia nchini kuelezea mambo mbalimbali ambayo yanahusu jumuiya ya SADC hasa utekeleza wa MPango mkakati wa kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na uchumi wa kati wa viwanda na amani.
0 Comments