📌MWANDISHI WETU
MWANDISHI wa Habari Ndg Mathias
Canal amechangia madawati 30 yenye thamani ya shilingi 2,100,000, na Vitakasa
mikono 20 vyenye thamani ya shilingi 1,400,000.
Ametoa mchango huo leo tarehe 29
Septemba 2023 wakati akizungumza kwenye mahafali ya 60 ya shule ya msingi
Kiomboi Bomani iliyopo katika kata ya Kiomboi, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Pamoja na mambo mengine pia Ndg
Mathias amechangia kwa kutoa motisha ya shilingi 500,000 kwa ajili ya walimu
katika shule hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kuwafundisha
wananfunzi shuleni hapo.
Kadhalika amesema kuwa
atawasomesha Watoto wote watakaomaliza darasa la saba na kupata ufaulu wa alama
‘’A’’ kwa kila somo kuanzia wale waliohitimu mwaka huu 2023 katika shule hiyo.
Katika hatua nyingine
amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi shuleni hapo kwa kukubali kuchangia
kwa hiyari baadhi ya mahitaji ya wanafunzi ikiwemo chakula kwa ajili ya
wanafunzi ambao wapo katika madarasa ya mitihani.
Ameongeza kuwa wanafunzi hao bado
hawajamaliza elimu ya darasa la saba mpaka pale watakapopata matokeo ya
mitihani waliyoifanya hivyo wazazi na walenzi wanapaswa kuendelea kuimarisha
ulinzi na mwenendo bora wa malezi kwa watoto hao.
Pia Mwandishi Mathias Canal
ameipongeza serikali kwa kutoa shilingi Mil 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba
vya madarasa Pamoja na ofisi ya walimu.
Katika mahafali hayo Mwandishi
Mathias Canal aliambatana na Diwani wa kata ya Kiomboi Mhe Omary Omary, na
Mkurugenzi wa DM PLANET Ndg David Mtengile ambaye amechangia 100,000 kwa ajili
ya motisha kwa walimu.
0 Comments