MIKOA SITA KUPEWA CHANJO YA POLIO

 ðŸ“ŒRUCIANA NYONI.

WIZARA ya Afya imeendelea kushirikia na Ofisi ya Rais TAMISEMI  na wadau mbalimbali katika kutekeleza  afua za kukinga na kuthibiti na kukabiliana na magonjwa ikiwemo  magonjwa yanayozuilika kwa chanjo nchini kama  polio,Rubella na Surua.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 8.  2023 jijini Dodoma na Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Katika kipindi cha miaka mitatu (3)  nchini Tanzania  kama ilivyo kwa mataifa mengine ilikabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeleta athari  kadhaa kwa afua  zingine za afya ikiwemo mwitikio wa chanjo mbalimbali nchini hasa kwa mwaka 2020 hadi 2022.

Hali hii imepelekea kuanza kwa visa na mlipuko wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambayo yalikuwa yamedhibitiwa ikiwemo ugonjwa wa Surua, Rubella na polio.

Kwa mara ya mwisho mgojwa wa polio aligundulika nchini mwaka 1996 hivyo shirika la afya duniani (WHO) lilitangaza Tanzania kuwa nchi isiyo na maambukizi  ya ugonjwa wa polio mnamo mwezi Novemba 2015.

Mnamo 26 Mei 2023, Wizara ya afya ilipokea taarifa uwepo wa mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja ambaye alionyesha dalili za kupooza kwa ghafla. Mtoto huyo  alitolewa taarifa  kutoka Manispaa ya Sumbawanga  Mkoa wa Rukwa uchunguzi wa maabara  ulisibithisha  kuwa mtoto huyo  ana maambukizi wa virus ya polio"  amesema Ummy Mwalimu

Aidha  Wizara ya Afya imekuwa ikifuatilia mwenendo wa magonjwa hayo  na kutoa taarifa kwa Umma mara kwa mara kusisitiza hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kukinga, kudhibiti na kukabiliana na magonjwa hayo.

Wizara ya afya inawahimiza wananchi kuendeleza kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa polio kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya kwa kufanya yafuatayo kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya mara tu unapoona dalili za kupooza kwa ajili ya uchunguzi na matibabu, kunawa maji tiririka na kwa sabuni, matumizi sahihi ya vyoo bora na kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo kulingana na ratiba ili kuwakinga dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo

Ummy mwalimu. 

Wizara ya afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wadau wa chanjo imefanya maandalizi kwa ajili ya kuwezesha zoezi hilo bila kuathiri shughuli zingine za wananchi.

Kampeni maalumu ya utoaji wa chanjo ya matone dhidi ya polio ( nOpv2) kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka nane (8) kampeni  hiyo itafanyika kwa siku nne ( 4) kuanzia tarehe 21-24 Septemba 2023  katika Mikoa (6) inayopakana na nchi zenye mlipuko wa polio ambayo ni Mkoa Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya.

Post a Comment

0 Comments