MIKAKATI WIZI WA FEDHA AFRIKA YAWEKWA

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

KATIKA kuhakikisha utoroshaji wa Mali za Afrika unakoma baada ya kubainika kuwa Malighafi nyingi zimekuwa zikienda kwenye mataifa ya nje na Fedha nyingi zikipotea kwenye mikataba huku ukwepaji wa kulipa kodi kwa wawekezaji likiwa ni dondandugu..

Kutokana na hali hiyo wabunge wa Chama Maalumu wanaojihusisha na kupambana na utoroshaji wa Fedha na ukwepaji wa Kodi kwa Tanzania na Afrika kikao kilichowakutanisha Watu wa Mataifa chini ya sabu Sahara Zimbabwe, Afrika kusini, Zambia Malawi, Kenya, Uganda na Tanzania.

Akiongea mara baada ya kuzindua kwa Chama hicho jijini Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Azzan Zungu amesema lengo la mkutano huo ni kujiwekea mikakati katika kuzishauri serikali zao ni jinsi gani zitaweza kudhibiti wizi wa pesa zinazoenda nje kama biashara haramu.

Chama hichi kimeanzishwa ili kuazisha mkakati maalumu kwa mataifa yote ya Afrika kuanza kupambana na utorishaji wa Fedha kwenda nchi za nje

Nchi za Afrika ziongeze thamani kwa malighafi zinazohitajika nje viwanda vifunguliwe na mali ziongezwe thamani kabla ya kusafirishwa nchi za nje badala ya kuondoka kama thamani mbichi kwenda nchi nyingine

Kwa kufanya hivyo tunapeleka Ajira katika nchi za wenzetu na mapato tunagawana madogo jambo ambalo Fedha zingeweza kubaki nchini kwetu kwa kuziongezea thamani

Zungu.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu kutokea Mkoa wa Shinyanga Salome Majamba pia mwanachama wa Mtandao wa wabunge unahusisha na kupambana na utoroshaji wa Fedha na ukwepaji wa Kodi kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Amesema mpaka wameamua kuunda kikundi hicho Cha wabunge vinara Katika kupambana na Hali hiyo ni wazi kuwa Hali ni mbaya.

Mfano kwa kila Dola 10 ambayo inaingia nchini kwa msaada kutoka nchi  mbalimbali Dola tisa  inaondoka nchini kwa kupitia utoroshaji wa Fedha au Ukwepaji  wa ulipaji kodi.

Kwani kwa kufanya hivyo moja kati ya kazi na majukumu ya kikundi chao ni kuikumbusha serikali kutunga Sheria ngumu zitakazoweza kuwabana wale wanaotorosha Fedha na kukwepa kulipa kodi kwa wawekezaji.

Pili kuikumbusha serikali kusimamia Sheria zilizopo ili ziweze kuwanufaisha Watanzania kwa rasilimali zilizopo.

Mimi Mbunge nitatimiza wajibu wangu katika kusimamia na kuishauri serikali Katika njia gani ya kudhibiti utoroshaji wa Fedha Watu wanaokwepa kulipa Kodi ili mtanzania aweze kunufaika.

Mkurungezi Mtendaji Policy  forum Semkae Kilonzo amesema Sababu ya kuzindua kwa Mtandao huo Ni kudhibiti utoroshaji wa Fedha zinazotoka kiharamu kwani kila Mwaka karibia Dola million 50 Hadi 80 zinapotea kutoka kwenye bara letu nchi nyingi zimekuwa zikiathirika kwa ukosefu wa Fedha za shughuli za Maendeleo na kuleta huduma yenye tija kwa wananchi.




 

Post a Comment

0 Comments