MBUNGE KATANI ATAKA ILANI YA UCHAGUZI 2020 IZINGATIWE KWA UJENZI WA KIWANGO CHA LAMI WA BARABARA KUTOKA MTWARA-NANYAMBA-TANDAHIMBA-NEWALA HAFI MASASI

 

📌SAIDA ISSA

IMEELEZWA kuwa ujenzi wa barabara ya Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala – Masasi yenye urefu wa kilometa 210 unatekelezwa kwa awamu ambapo ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mtwara – Mnivata (km 50) umekamilika kwa kutumia fedha za ndani. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani alipouliza 

Je, ni lini ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara kutoka Mtwara – Nanyamba –Tandahimba – Newala hadi Masasi ambayo ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi 2020 na ahadi ya Mhe. Rais itaanza ikizingatiwa kuwa upembuzi yakinifu umeshafanyika.

Alisema kuwa kwa sehemu ya Mnivata – Newala - Masasi (km 160) mikataba miwili ya ujenzi chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesainiwa tarehe 21 Juni, 2023 kwa sehemu za Mnivata – Mitesa (km 100) na Mitesa – Masasi (km 60) pamoja na ujenzi wa Daraja la Mwiti. 

Ambapo kwa sasa Wakandarasi wa sehemu zote mbili wapo katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi.

 

Post a Comment

0 Comments