MAKAMU wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt Philipo
Isidor Mpango amewataka
maafisa ustawi wa
jamii kufanya kazi
kwa weledi na kuzingatia
sera, sheria na miongozo
mbalimbali ya utoaji
wa huduma za
ustawi wa jamii
ili kuwezesha utoaji
wa huduma bora.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko wakati akifungua mkutano
mkuu wa mwaka
wa utendaji wa
maafisa ustawi wa
jamii nchini Jijini Dodoma
Septemba 6, 2023 kwa niaba ya Makamu wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt Philipo
Isidor Mpango
Naelekeza maafisa ustawi wa jamii kote nchini kuendelea kutoa elimu ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa jamii ili kupunguza au kutokomeza vitendo vya ukatili kwenye makundi mbalimbali ya kijamii, hii ni kutokana na ushahidi unaoonesha kuwa afya duni ya akili huchangia vitendo vya ukatili
Biteko.
Ni rai yangu kwa viongozi wa dini zote na wazee wa mila kuendelea kukekemea vikali matendo maovu katika jamii yetu na kufundisha mema, Ni imani yangu kuwa endapo waumini wa dini mbalimbali watazingatia mafundisho ya dini zao ustawi wa jamii yetu utaimarika kwakuwa na familia bora zenye watoto waliolelewa na kufundishwa maadili mema
Naye Waziri
wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalumu amesema
kuwa vituo vinavyohusika na
kutoa huduma za
ustawi wa jamii
ni pamoja na
Vituo vya huduma
za ustawi katika
Mikoa na halmashauri,vVituo vya kutolea
huduma za afya,
mahabusu za watoto, shule za
maadilisho, makao ya watoto, vituo
vya kulelea watoto
wadogo mchana, Nyumba salama, Vituo
vya mkono kwa mkono, Mahakama, Magereza, Taasisi na
Vyuo vya Elimu
ya Juu , Shule za
Msingi na Sekondari, maeneo yote
ya kazi , Taasisi za
dini pamoja na
maeneo yote yenye
kuleta mahusiano kati
ya mtu, familia
na jamii yote
kwa ujumla.
Maafisa Ustawi wa jamii waliuohudhuria katika mkutano huu ni wale ambao wanafanya kazi katika taasisi binafsi na Serikalini kwa maana ya Halmashauri, Wizara za kisekta na Taasisi za Umma na Sekta Binafsi. Aidha Maafisa hawa ni wale waliosoma kada za Ustawi wa Jamii, Sosholojia, Saikolojia, Unasihi na ushauri, Malezi na Makuzi, Ulinzi wa kijamii na Gerentolojia ya kijamii
Gwajima.
0 Comments