SERIKALI imezitaka Halmashauri
ziendelee kutenga na kutoa fedha shilingi 1,000 Kwa kila mtoto chini ya miaka
mitano kwa asilimia 100 au zaidi kwaajili ya utekelezaji wa afua za lishe.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Deogratius Ndejembi kwa niaba ya Waziri Mohamed Mchengerwa alipokua akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu cha kumbukumbu za sauti za walengwa wa mradi wa USAID lishe endelevu Jijini Dodoma Septemba 25,2023.
Mhe. Ndejembi amezitaka kusimamia kikamilifu utekelezaji wa masuala ya lishe kama yalivyobainishwa katika mpango jumuishi wa lishe wa mwaka 2021/22 mpaka 2025/26
Halmashauri zihakikishe zinaendelea kutoa motisha kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwani wao ndio nguzo kubwa ya utekelezaji wa afua za lishe
Ndejembi
Aidha Ndejembi amewataka viongozi wa serikali na chama kuhakikisha suala la lishe linatiliwa mkazo na kusimamiwa ipasavyo kama ambavyo imeelekezwa katika mkakati wa pili wa kitaifa wa kuboresha hali ya lishe (NMNAP II).
Maafisa lishe, Maafisa kilimo na mifugo mmejengewa uwezo na mmepewa vitendea kazi, wasaidieni wananchi kutumia mbinu bora za kilimo na ufugaji lakini pia hakikisheni wananchi wetu wanatumia mazao hayo kula ili kuboresha Afya na lishe ya familia zao
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania, Angela Kauleni amesema Takwimu za hivi karibuni za tathimini ya hali ya Afya na makazi (TDHS 2020) zinaonesha kuwa watoto 30 kati ya 100 walio chini ya miaka mitano wanakabiliwa na udumavu ambapo hali hiyo huathiri ukuaji na kupevuka kiakili, kimwili na kisaikolojia kwa watoto.
Pia amesema kama shirika wataendelea kushirikiana na serikali kutekeleza malengo na mipango ya kimikakati ya maendeleo na hasa inayolenga kuzuia udumavu na vifo vya watoto chini ya miaka mitano, upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote, ulinzi wa watoto na ustawi wa haki za watoto.
Ili kufanikisha malengo haya Save the Children itazingatia vipaumbele vifuatavyo- kukuza sauti na ushiriki wa watoto na jamii katika masuala yanayowahusu, kuimarisha uhusiano wa kimkakati na wadau mbalimbali kuwekeza kwenye mipango na tafiti zinawezesha jamii na taifa kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi
Kauleni
0 Comments