JOEL Hans Embiid ni mchezaji wa kikapu anayeshiriki
ligi kuu ya kikapu nchini Marekani maarufu kwa jina la NBA. Mchezaji huyo
aliyezaliwa nchini Cameroon mwenye uraia pacha wa Ufaransa na Marekani anayekipiga
katika klabu ya Philadelphia 76ers amezidi kutamba na tuzo yake ya mchezaji
bora ijulikanayo kama MVP (Most Valuable Player) ya mwaka 2023 baada ya
kuwapiku wachezaji kama Nikola Jovic, Giannis Antetokounmpo, Luka Doncic,
Jayson Tatum, Ja Morant pamoja na Lebron James ambao walikuwa katika
kinyang’anyiro cha tuzo ya MVP.
Akizungumza na vyombo vya habari alisema ni ndoto
kwake kupokea tuzo kubwa kama hiyo na imekuwa furaha kubwa kwa familia pamoja
na kuleta heshima kwa klabu yake pamoja na kuongeza morali kwa wachezaji
wenzake na anachukulia kama nyongeza ya tuzo na ndoto zake sasa ni kushinda
kikombe cha ligi kwani timu ina wachezaji wazuri wanaomzunguka na kila mtu yupo
tayari kuonja furaha ya kutwaa ubingwa wa NBA.
Mchezaji huyo aliongezea kwa sasa yupo vizuri kiafya
na baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi ya kikapu ameelekezea nguvu zake
kufanya mazoezi binafsi pia amesema katika kipindi hiki cha mapumziko
anatarajia kuwa karibu na mke wake Anne De Paula ambaye amefunga nae ndoa
tarehe 22 Julai 2023 na mwanamke huyo mwanamitindo wa Brazil mwenye makazi yake
New York nchini Marekani.
Mchezaji huyo aliyewahi kukipiga katika timu ya Kansas
Jayhawks amefunguka yupo tayari kutoa tamko juu ya chaguo la timu ya taifa
ambayo ataitumikia kwenye mashindano ya kimataifa ila amesema mara baada ya
mashindano ya kimataifa ya FIBA kutamatika Septemba 2023.
Kuhusiana na usajili wala sina shaka kwani tetesi zinazoendelea za mimi kutimkia Oklahoma City Thunder ni za uzushi, mimi nina mkataba wa miaka minne na 76ers ambao unatarajia kuisha 2026 na ninafuraha ndani ya klabu yangu pia bado tuna malengo ya muda mrefu na kocha Glen Antony (Doc Rivers)
Embiid.
Embiid anayejulikana kwa jina la utani `The Process’
aliyeibuka mfungaji bora kwa kuongeza idadi ya vikapu vingi kwa misimu ya miaka
miwili mfululizo 2021-2022 na 2022-2023 na kujinyakulia tuzo ya NBA Scoring
Champion akiwa ni kiungo wa kwanza kufanya hivyo tangu Shaquille O’Neal mnamo
mwaka 2000 na kiungo Moses Malone mnamo mwaka 1982 akiwapiku wote kwa zaidi ya
pointi 30 kama raia wa kigeni.
0 Comments