📌 JASMINE SHAMWEPU
MKUU wa Mkoa Wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Septemba 26, 2023 amefungua kikao kazi cha kupitia Utekelezaji wa Mradi wa kuongeza Ustahimilivu wa Mabadiliko ya tabianchi na kuboresha mifumo ya ikolojia kilicho andaliwa na Shirika la CARE International katika Ukumbi wa Nyerere -Morena Jijini Dodoma
Akizungumza wakati wa kikao hicho amesema Mradi huo ni bora na wakuigwa kwa jamii hivyo ametoa rai kwao kuangalia namna ambayo itasadia kuongeza uwezo wa kutoa elimu ya Mazingira na kuzuia uharibifu utokanao na shughuli za kibinadamu na kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi na pia kuendelea kuboresha Sera, Mipango na Sheria zilizopo.
Aidha, Mhe.Senyamule amesema mbali ya athari za mabadiliko ya Tabia nchi shughuli za kibinadamu zimekuwa sehemu ya changamoto kwa kuchochea kuharibu ufanyaji kazi wa mfumo wa ikolojia kama vile ukataji miti, uvamizi wa misitu na uvunaji wa wanyama bila kufuata taratibu za uhifadhi, kulima kwenye vyanzo vya maji, kuvamia hifadhi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.
Hivyo vyote vimechangia kubadilisha utendaji wa mifumo ya ikolojia na huduma zake mfano upatikanaji wa maji ya uhakika, ardhi kutokuwa na rutaba, mmomonyoko wa udongo, kupotea kwa baadhi ya spishi za mimea ama wanyama.
Senyamule
Mhe. Senyamule amesema Mradi huo utatekelezwa katika Wilaya tano za Kiteto, Simanjiro, Same, Chemba na Wilaya ya Mufindi ambapo Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara wamekutana ili kuona nini kimepangwa kwenye Mradi na jinsi gani wataweza kushiriki kwani wao ndio walengwa wa moja kwa moja kwa kushirikiana na wanajamii.
Naye, Kaimu Mkurugezi Mkaazi wa Shirika la CARE Tanzania Bi.Haika Mtui amesema lengo la Mradi huo ni kufanya mifumo ya ikorojia kuweza kutoa huduma sahihi katika kuboresha chakula ili jamii iweze kutumia rasilimali , kujiongezea kipato chao pamoja na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na kutunza Mazingira
Kwa Upande wake, Kaimu Mkurungezi wa Wilaya ya Chemba Bw. Said Sambala amesema kupitia kupitia Mradi huo wanakwenda kuboresha suala la mazingira na kuwafikia wakulima wengi kwa kuwawezesha kuwa na kipato pamoja na kujitosheleza kwa chakula.
0 Comments