ANWANI ZA MAKAZI ZITAWEZESHA TATHMINI YA HARAKA: SHEKIMWERI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabiri Shekimweri amesisitiza kuundwa kwa Timu ya ufuatiliaji na tathmini ya zoezi la Anwani za Makazi ili kufanikisha azma ya Serikali ya kila mtu kutambulika kirahisi mahali anapoishi kwa lengo la kufikiwa na huduma za Kijamii kwa haraka.

DC Shekimweri ameeleza hayo  leo Jijini Dodoma, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo kuhusu Mfumo wa anwani za Makazi kwa Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Maafisa Watendaji wa Mitaa wa Jiji la Dodoma ambayo yameandaliwa na wizara ya Habari, Mawasiliano na teknolojia ya Habari .

Aidha, katika hatua nyingine DC Shekimweri amewataka Maofisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuwa anuani za makazi ni hitaji la msingi kwasasa kutokana na kukua kwa teknolojia nchini.

Kwa sasa hivi ni rahisi kuita gari la kukodi (Uber) ukaonesha eneo unapokwenda na huduma hiyoikakufikia, hivyounaweza kuita huduma ukiwa nyumbani kwako

DC. Shekimweri

Pia ametoa wito kupitia vikao vya kisheria ikiwamo Mabaraza ya madiwani kupewa muda wa kuwasilisha elimu ya suala hilo na wajibu wao wa kuhamasisha wananchi kujisajili na mfumo wa anwani za makazi

Kwa upande wake Mratibu wa Anwani za Makazi Kitaifa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Jampyon Mbugi, amesema hadi sasa Jiji la Dodoma limekusanya taarifa na kutoa anuani za makazi 245,000 kati ya hizo 163,000 ni za majengo na 81,277 ni viwanja vitupu.

Wananchi 299,330 ndio waliosajiliwa kwenye mfumo wa anwani za makazi, idadi hii haiakisi uhalisia wa takwimu za idadi watu waliopo ndani ya Jiji la Dodoma inayokadiriwa kuwa zaidi ya 765,000

Amesema kuwa zaidi ya wananchi 465,849 hawajasajiliwa kwenye mfumo huo na hivyo serikali imeamua kuongeza msukumo wa suala hilo hususani kwa kutumia Wenyeviti, Watendaji wa Kata na Mitaa.

Dhamira ya Wizara ni kuhakikisha Dodoma inakuwa ya mfano na kuwa chachu kwa halmashauri zingine kuja kujifunza namna ya kufanikisha utekelezaji wa mfumo huo.

Mhandisi Mbugi.



 

Post a Comment

0 Comments