MKURUGENZI Mkuu wa
Tume ya nguvu za Atomu [TAEC], Prof Lazaro Busagara ametoa wito kwa wananchi
kuacha kutumia baadhi ya vitu/malighafi bila ya tume ya nguvu za atomu kuvipima
kujihakikishia kama vina mionzi ili kulinda afya za watu.
Ameyasema hayo alipokua akizungumza na Balozi wa Tanzania-Austria, pamoja na vyombo vya habari Agosti 31,mwaka 2023 jijini Dodoma ambapo alibainisha vitu hivyo ni kama vyuma chakavu, maji yanayochimbwa kutoka ardhini pamoja na vyakula.
Nipende kutoa wito kwa watanzania wenzangu wapende kutumia vitu vilivyopimwa na tume ya nguvu za atomu Tanzania ili kuepukana na madhara yatokanayo na mionzi. Tuna jumla ya vituo 52 vinavyohusika na upimaji wa vitu vyenye viasili vya mionzi
Prof Busagara
Naye Balozi wa
Tanzania-Austria Balozi Naimi Azizi amesema kuwa anawapongeza tume ya nguvu za
atomu kwa kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kuwafanya watanzania kuchukua
tahadhari.
Teknolojia ya nuclear ni mtambuka nashukuru kwa kazi kubwa mnayofanya kuwaweka watanzania salama, napenda kutoa ahadi mimi binafsi na ofisi yangu tutashirikiana na tume hii kuhakikisha yale malengo ambayo tume na serikali imepanga yanatimia
Balozi Naimi
0 Comments