WAKULIMA WA ZAZBIBU WAKUMBUSHWA KUFUATA USHAURI WA WATAALAMU

📌SUZANA ALEX

AFISA kilimo zabibu, Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) Ezekiel Kaponoke amesema  zabibu ni zao la biashara ambalo halina masharti sana na kama mkulima akifuata ushauri kutoka kwa wataalamu wa zao hilo anaweza kuzalisha mazao kwa wingi

Kaponoke ameyasema hayo leo katika viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma alipokua  akizungumza na waandishi wa habari

Zabibu zinaweza kustawi eneo lolote hasa Dodoma kwasababu hazihitaji maji mengi pia kwa utafiti wa kilimo tuliofanya mbolea ya samadi ni mbolea inayostahili ambapo inakaa kwa muda wa miaka 5  kuliko kutumia mbolea za viwandani ambazo zinafanya mmea ukue kuelekea juu

Kaponoke

Kwaupande wake Aloyce Haule mkazi wa Kikuyu kaskazini ambaye ni mkulima wa zabibu Mpunguzi amesema zabibu ni zao ambalo halina gharama katika ukuaji wake.

Mmea wa zabibu unaanza kutoa matunda yake kwa muda wa miezi 15 mpaka18 na ukishaanza kutoa matunda unakua unavuna tuu kwani mimea ina uwezo wa kukaa mpaka miaka 20 ikiwa inatoa matunda tuu

Haule.

Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kutokana na utafiti iliyofanya imethibitisha mazao kama zabibu, alizeti mtama na uwele ni mazao yanayoweza kulimwa maeneo yenye mvua chache hasa Kanda ya kati.

 

Post a Comment

0 Comments