WAFANYABIASHARA
katika soko la Sabasaba Mkoani Dodoma wameiomba serekali kuwarudishia stendi ya
Daladala iliyohamishiwa katika soko Machinga Complex ili kuweza kunusuru
biashara zao.
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumzia na waandishi jijini Dodoma wafanyabiashara hao wamesema baada ya serikali kuhamisha huduma hiyo wateja wengi wamepotea tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Mwajuma Ramadhani amesema kuwa stendi katika soko la sabasaba ina umuhimu sana kwa kuwa inaleta wateja katika soko hili
Daladala ni muhimu katika soko hili kwa sababu wateja wengi hawafiki katika soko hili kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa kubebea bidhaa zao na hivyo kwenda katika soko ambalo liko jirani na usafiri
Pia soko ni kubwa na biashara imekuwa ngumu kutokana na uhaba wa wateja naiomba serikali ituludishie standi katika soko hili
Mwajuma
Akizungumza ofisini kwake Makamu Mwenyekiti wa Soko hilo Kombo Adam Kombo amesema kuwa stendi hiyo ilihamishwa baada ya Waziri Mkuu kumuagiza Mkuu wa Mkoa kuiondoa, hivyo wao kama uongozi wa soko walienda kuomba irudishwe kwani abiria wa daladala ndiyo wateja wao.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa sisi binafsi tulihuzunika na tulijaribu kuchukua hatua za kuwasilian na na viongozi wa serekali mpaka viongozi wa chama namna ya kuweza kujeresha stendi kwasasabu stendi hii ilikuwa inaunganisha watu fofauti tofauti kutoka maeneo mbalimbali.
0 Comments