VIVUTIO UTALII VYAWAVUTIA WAKAZI DODOMA MAONESHO NANENANE

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WAKATI maonesho ya wakulima nanenane yakiwa yamefikia kilele baadhi ya wakazi wa Dodoma wamewaasa wananchi wengine kushawishika kutembelea maeneo ya hifadhi za wanyamapori ili kujifunza maisha ya wanyama.   

Wakizungumza siku ya kilele cha 88 kwenye viwanja vya nzuguni jijini Dodoma baadhi ya wananchi waliotembelea maonesho hayo wamesema kuna mambo mbalimbali wamejifunza ikiwamo tabia za wanyamapori na kuwashawishi wengine kutembelea hifadhini.

Kama pale nimeona simba ana uwezo ukubwa kilo 250, nilikuwa nashangaa anawezaje kumuangusha nyati kumbe ni mkubwa sana, nawahimiza wananchi wengine hata kama maonyesho yameisha wajitahidi kutembelea hifadhi zetu

Mela Mabula

Kwa upande wake Afisa mhifadhi wa bodi ya utalii George Mwagane amesema kwa sasa wameingia mikoa ya kanda ya kati kwa ajili ya kuhamasisha utalii kwa wananchi kutembelea hifadhi zilizopo nchini ili kujionea wanyama mbalimbali.

Tunaona wananchi wengi wamevutiwa na maonesho ya wanyamapori hivyo tunawahamasisha wakazi wa Dodoma na mikoa ya kusini kuanza kutembelea hifadhi zetu ili kumuunga mkono Mama Samia Suluhu kwenye filamu ya Royal Tour

George Mwagane

 

 

Post a Comment

0 Comments