VIJANA NDIO WENYE NAFASI YA KULIJENGA TAIFA.

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

BALOZI wa Marekani nchini Tanzania Michael Balton amesema vijana wa kitanzania ndiyo wenye nafasi kubwa ya kulijenga taifa lao kwa namna wanavyotaka liwe hapo badaye.

Aidha amewataka vijana nchini kutumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumini na kuacha kufanya mambo kwa kuigia mila na desturi za mataifa mengine ambazo haciendas tamaduni zao.

Balozi Balton, ameyasema hayo kwenye Kongamano la vijana na demokrasia lililofanyika jijini Dodoma

Amesema vijana wa kitanzania ndiyo wenye nafasi ya kuamua taifa hili liwe la namna gani hapo baadaye kutokana na nguvu kazi iliyopo kwa Kundi hilo nchini.

Vijana mnapaswa kutambua kuwa nyinyi ndiyo wenye jukumu la kulitengeneza taifa hili liwe na namna gani hivyo mnapaswa kuwa sehemu kubwa ya kulijenga taifa hili ili liwe imara au vinginevyo

Balozi Balton

Kadhalika, amesema vijana wanapaswa kufanya mambo yao kwa mujibu wa mila na desturi za taifa lao na kuacha tabia ya kuiga tamaduni za mataifa mengine.

Naye mgeni rasmi katika kongamano hilo Mwenyekiti wa Bunge David Kihenzile, amesema vijana wanapaswa kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zitolewa na serikali na kuacha kulalamika vijiweni.

Amesema Tanzania ina rasirimali nyingi ambazo kama zitatumiwa vizuri na vijana zinaweza kuwakwamua kiuchumi na kupunguza malalamiko ya uhaba wa ajira nchini.

Tanzania ina madini mengi, mifugo mingi lakini pia ardhi kubwa ambayo inafaa kwa kilimo hivyo vijana kama watatumia vizuri rasirimali hizi wataweza kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato

Vile vile amesema ipo haja kwa taifa kuanza kuandaa vijana ambao watakuja kuliongoza taifa hili kwa misingi ya uadilifu.

Lazima kama taifa tuwe na watu ambao watakuja kuliongoza taifa hilo ambao wataweza kulinda rasirimali zetu hivyo lazima kuwa na vijana ambao wana elimu ya kutosha,waadilifu,wazalendo na wanao lijua taifa lao ipasavyo

Kihenzile 

 

Post a Comment

0 Comments