MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkundwe Mwasaga amesema kuwa kuelekea mwaka wa fedha 2023/2024 Tume hiyo itaendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar.
Ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Agosti 25, mwaka 2023 .
Kuwezesha uanzishaji wa vituo vya majaribio ya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation Hubs) katika Wilaya 10 na kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA kwa kila Wilaya
Mwasaga
Aidha amesema kuwa Tume hiyo ipo na mpango wa kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly Center)
Kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini
Mwasaga
Pia amesema Tume hiyo itawezesha mafunzo maalumu ya wataalamu wa TEHAMA 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.
0 Comments