TUME YA MADINI YASEMA MASOKO YA MADINI YASAIDIA KUZUIA UTOROSHAJI WA MADINI YA DHAHABU

 ðŸ“ŒJACKLINE VICTOR

Dodoma:  Sekali kupitia Tume ya Madini imesema kuanzishwa  kwa masoko ya madini kumesaidia kuzuia utoroshaji wa madini ya dhahabu kwenda nje ya nchi. 

Haya yameelezwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Madini kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na mikakati ya mwaka 2023/2024. 

Ukiangalia kabla ya uanzishwaji wa masoko wachimbaji wengi walipata tabu kujua dhahabu yao wanaipeleka wapi. Kipindi cha nyuma wakati hatuna masoko ilikuwa ni vigumu sana kupata takwimu za uzalishaji wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Masoko yametusaidia mno, siwezi kusema kwa asilimia ngapi kuzuia utoroshaji wa dhahabu. Tunaweza tukakubali kwamba  wachimbaji wadogo kupitia masoko tumeweza kukusanya bilioni 157   kama mrabaha na ada ya ukaguzi wa madini nchini sawa na asilimia 23.22 ya makusanyo yote yaliyokusanywa na tume kwa mwaka husika.”amesema Mhandisi Lwamo.  

Uanzishwaji masoko ya madini una lengo la kuimarisha udhibiti wa biashara ya madini nchini ili kuongeza mapato yatokanayo na rasimali madini kwa Serikali. 

 

Post a Comment

0 Comments