TAASISI ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima na jamii kutumia mbegu zilizothibitishwa ubora ili kuongeza mavuno, tija na kipato.
Mkurungezi Mkuu wa TOSCI, Patrick Ngwediagi, ameyasema hayo leo Agoti 15 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema ili kilimo kuwa na tija nchini wakulima wanapaswa kutumia mbegu zenye ubora na zilizothibitishwa na taasisi hiyo ili kuongeza mavuno na kipato.
Wito wangu kwa wakulima na jamii kwa ujumla tumieni mbegu zilizothibitishwa ubora ili kuongeza mavuno, tija na kipato badala ya kuendelea kutumia mbegu ambazo hazina ubora na kupunguza tija kwenye kilimo nchini
Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 amesema watatumia kiasi cha Sh.bilioni 12.6 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
Amesema moja shughuli watakayoifanya ni kuendelea na uboreshaji wa shughuli za utafiti na usimamizi wa ubora wa mbegu.
Taasisi itaendelea kuboresha shughuli za uthibiti na usimamizi wa ubora wa mbegu zilizoanzishwa katika mwaka wa fedha uliopita katika maeneo mbalimbali
Kadhalika amesema shughuli nyingine ni kuteleza mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi (AFDB) kwa kujenga maabara yenye uwezo mkubwa.
Maabara hii itawezesha taasisi kufanya uchambuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu mbegu katika makao makuu ya TOSCI
Aidha, amesema pia wamepanga kujenga maabara ya mbegu kwenye tawi la taasisi hiyo kanda ya ziwa mkoani Mwanza .
Pia kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuelimisha umma juu ya matumizi ya mbegu zilizothibitishwa ubora za zenye lebo ya TOSCI.
Kuthibitisha na kusimamia ubora wa miche/vipando na pingili za mazao ya miti ya matunda, migomba na miwa
Hata hivyo, amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita taasisi hiyo imesajili zaidi ya aina za mbegu 647 na kuwachukulia hatua watu wote waliobainika kuuza mbegu feki kwa kuwafikisha Mahakamani.
0 Comments