📌RHODA SIMBA
SAMPULI 70 za asali ya Tanzania kutoka wilaya 34 zilizopelekwa kwenye maabara ya kimataifa iliyopo nchini Ujerumani matokeo yalionesha kuwa asilimia 96 ya sampuli hizo zilikidhi viwango vya ubora wa Kimataifa.
Mafanikio hayo yamebainishwa na Kamishina wa Uhifadhi wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo jijini Dodoma Agosti 16, 2023, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TFS kwa mwaka 2022/2023 pamoja na vipaumbele vyao kwa mwaka 2023/2024
Prof. Silayo amesema kuwa kupitia mashindano ya ubora wa asali zinazozalishwa Barani Afrika, asali ya Tanzania iliyozalishwa mkoani Tabora ilishika nafasi ya pili kwa ubora na asali ya Tanzania imeendelea kuuzwa katika masoko ya nchi za Umoja wa Ulaya, Uarabuni na kwenye masoko mapya ya Poland na China.
Amesema kuwa TFS inasimamia hifadhi za nyuki 20 zenye ukubwa wa hekta 39,444 na kwamba nchi inakadiriwa kuwa na makundi ya nyuki (bee colons) takribani milioni 9.2. Uzalishaji wa mazao ya nyuki umeongezeka ambapo kwa sasa wastani wa tani elfu 33 huzalishwa kwa mwaka.
Kama sehemu ya jitihada za kuongeza tija katika ufugaji nyuki nchini TFS ilianzisha mashamba 3 ya nyuki (Bee Farms) Shamba la nyuki la Kipembawe katika Wilaya ya Chunya lenye ukubwa wa hekta 20,728, pia umeendeleza mashamba ya Nyuki ya Mwambao (Handeni – Kilindi) na Kondoa-Manyoni lililopo katika Wilaya za Kondoa na Manyoni kwa kuanzisha manzuki mpya 14
Prof. Silayo
Prof Silyo ameongeza kuwa Wakala umetoa elimu ya ufugaji bora wa nyuki kwa wafugaji nyuki 1,998 kutoka katika vijiji 40.
Wakala umeanzisha mfumo unaoitwa “Honey Traceability System” ambao unafuatilia ubora wa asali kuanzia kwa mfugaji hadi pale inapoingia sokoni.
0 Comments